Lugangira: Tunahitaji ulinzi wa mbegu za asili

DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum, Neema Lugangira ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa hatua ya kutambua mbegu za asili na kuamua kujenga benki ya hifadhi ya mbegu (gene bank) nchini, hatua ambayo amesema itasaidia kupunguza utegemezi wa mbegu kutoka nje, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuchangia lishe bora kwa wananchi.

Akichangia mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, leo Mei 22 Lugangira alitoa mapendekezo kadhaa kwa Serikali ili kuimarisha zaidi sekta ya mbegu nchini.

“Ni muhimu Sera ya Mbegu ikatambua na kutoa ulinzi kwa mbegu za asili za wakulima. Vilevile, tunahitaji Sheria ya Mbegu itambue haki ya wakulima katika kutumia na kuhifadhi mbegu zao,” alisema.

Mbunge huyo alisisitiza umuhimu wa kukamilisha mchakato wa National Plant Genetic Resources for Food and Agriculture (NPGFRA) ambao utalinda haki za wakulima kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa UNDROP.

Akihimiza kuimarishwa kwa mifumo ya hifadhi ya mbegu, Lugangira alipendekeza kujengwa kwa benki za mbegu za asili katika kila mkoa ili kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora na zinazofaa kwa mazingira husika.

Aidha, aliiomba Serikali kuhakikisha zao la vanilla linapatiwa soko la uhakika ili kuwawezesha wakulima wa zao hilo mkoani Kagera kunufaika. Alisisitiza pia umuhimu wa kuwekeza katika eneo la tafiti kwa kuongeza bajeti ya tafiti ndani ya sekta ya kilimo.

Katika bajeti hiyo, Wizara ya Kilimo Bunge liliidhinisha jumla ya shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kilimo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now, YOU can too with the Home Profit System:

    ACT NOW➢ https://Www.Earnapp1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button