Lugumi awajengea ghorofa watoto wenye uhitaji

DAR ES SALAAM :Mfanyabiashara Said Lugumi amejenga na kukabidhi majengo saba ya ghorofa 4 kwa ajili ya kulea watoto zaidi ya 800 waliopo Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni katika kusaidia kundi hilo ambalo linahitaji makazi ya pamoja na malezi.
Akizungumza leo wakati wa kukabidhi moja ya jengo la ghorofa nne lililopo eneo la Kinondoni Shamba, Lugumi amesema majengo yote saba yatakamilika Machi 2025 na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya maradhi kwa watoto watokao mazingira magumu.
Aidha, Lugumi amesema licha ya kukabidhi majengo hayo pia amejitolea kuwasomesha watoto hao zaidi ya 800 kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi chuo kikuu ili kuwajengea maisha bora ya baadaye.