DODOMA: WANAWAKE wa Wizara ya Nishati, wameungana na wanawake wenzao duniani kuadhimisha siku ya wanawake ambayo mkoani Dodoma imeadhimishwa wilayani Chamwino.
Katika madhimisho hayo watumishi wametumia siku hiyo kuelimisha wananchi mbalimbali kuhusu nishati safi ya kupikia.
Akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi Joyce Msangi Ofisa Misitu, alisema utumiaji wa nishati safi ya kupikia unalinda afya za walaji na inamuepusha mtumiaji na madhara mbalimbali.
Aliyabainisha madhara hayo, ni pamoja na adhari kwenye mfumo wa upumuaji na inaharibu mazingira.
Naye, Talkisia Erio Ofisa Kumbukumbu, amewahimiza wanawake wa Dodoma kutumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Katika Madhamisho hayo, yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Chinagali Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima.