‘Maamuzi sahihi hayaishii pale msimu wa sikukuu unapoishia’

Dar es Salaam: Ingawa msimu wa sikukuu umefikia tamati, umuhimu wa unywaji kistaharabu na usalama barabarani unaendelea kuwa mkubwa, hususani katika mwezi wa Januari ambao huja na changamoto zake.

Watanzania wengi wanapokuwa wanarejea kazini baada ya safari za mikoani wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, matumizi ya barabara hubaki kuwa makubwa. Kipindi hiki pia huambatana na vinywaji vya baada ya kazi, mikusanyiko ya wikendi na mahangaiko ya kijamii yanayoweza kufanya watu kupuuza tahadhari.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Serengeti Breweries Limited (SBL) imeungana na Bolt kuhamasisha maamuzi salama baada ya shughuli za kijamii na kupunguza hatari zinazotokana na uendeshaji wa magari ukiwa umelewa. Ushirikiano huu unaunganisha programu ya SBL ya unywaji wa kimaadili, ‘Wrong Side of the Road (WSOTR)’, na huduma za usafiri za Bolt, ili kuwezesha upatikanaji wa usafiri salama na wa uhakika katika kipindi hiki cha mwendo mkubwa.
Kiini cha kampeni hii ni wito wa kuchukua hatua. Watanzania wanahimizwa kutazama video ya elimu ya ‘Wrong Side of the Road’, kukamilisha mafunzo na kupakia cheti chao ili kupata Sherehe Code, itakayowawezesha kufurahia punguzo la asilimia 30 kwenye safari za Bolt hadi tarehe 15 Januari. Aidha, washiriki watakuwa na fursa ya kuchaguliwa kupanda Special Bolt, gari maalum lenye chapa maalumu lililobuniwa kutoa uzoefu wa kipekee huku usalama ukiendelea kupewa kipaumbele.
Kupitia kampeni hii, ujumbe wa kuzingatia mazoea chanya ya unywaji unasisitizwa sio tu wakati wa sikukuu, bali kwa mwaka mzima. Haya yanajumuisha kula kabla ya kunywa, kunywa kwa kiasi, kubadilisha vinywaji vya pombe na maji, kuepuka kuendesha gari ukiwa umelewa, kupanga usafiri salama wa kurudi nyumbani, pamoja na kuwajali marafiki wanaoweza kuhitaji msaada.
Ushirikiano huu unaendeleza juhudi za mpango wa Wrong Side of the Road wa SBL, ulioanzishwa mwaka 2023 chini ya kampeni ya INAWEZAKANA, kuimarishwa mwaka 2024 kama Inawezekana kuwa mtu makini, na sasa unaendelea mwaka 2025 kupitia kauli mbiu ya Inawezekana Kabisa. Mpango huu unalenga kupunguza ajali zinazohusiana na matumizi ya pombe kwa kuhimiza maamuzi sahihi katika nyakati za kawaida za kijamii na vipindi vya msongamano wa usafiri.
Zaidi ya ujumbe, kampeni hii pia imeungwa mkono na elimu ya ana kwa ana. Wakati wa Tamasha la Nyama Choma, timu ya SBL ilikutana moja kwa moja na watumiaji, ikitoa elimu ya vitendo kuhusu unywaji wa kimaadili, ikiwemo kula kabla ya kunywa, kunywa taratibu, kunywa maji kati ya vinywaji vya pombe, na kuepuka kuendesha gari ukiwa umelewa. Maji pia yaligawiwa kama sehemu ya kuhamasisha unywaji wa kiasi, afya na ustawi wakati wa mikusanyiko ya kijamii.
Dhamira ya SBL katika kupambana na uendeshaji wa magari ukiwa umelewa haijaishia kwenye ushirikiano huu pekee. Katika mwaka wa 2025 pekee, zaidi ya watu 7,000 wamepatiwa elimu kuhusu madhara ya kuendesha gari baada ya kunywa pombe kupitia programu ya Wrong Side of the Road, ambapo washiriki walikamilisha mafunzo na kupokea vyeti. Kabla ya ushirikiano huu, SBL pia ilishirikiana na wadau muhimu wakiwemo LATRA na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kuonesha juhudi endelevu na za pamoja katika kuimarisha usalama barabarani.
Kampeni hii pia inaunga mkono jitihada za Serikali katika kulinda usalama na afya ya jamii. Kwa kuhimiza unywaji wa kimaadili na matumizi ya usafiri salama, Inawezekana Kabisa inachangia kupunguza ajali za barabarani, kupunguza mzigo kwa hospitali na huduma za dharura, na kuboresha ustawi wa jamii kote nchini.
Akizungumza wakati wa kutangaza ushirikiano huo, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu, alisema ushirikiano huo unaakisi wajibu wa kampuni kwa jamii inazozihudumia.
“Januari ni kipindi ambacho watu wanarejea katika ratiba zao za kawaida, lakini shughuli za kijamii na unywaji vinaendelea, na hatari bado zipo. Kupitia ushirikiano wetu na Bolt, tunawakumbusha watu kuwa burudani na uwajibikaji vinaweza kwenda pamoja, si wakati wa sikukuu pekee bali kila siku. Tunataka kila mmoja afanye maamuzi salama na afike nyumbani salama.”
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Bolt Kanda ya Tanzania, Kenya na Uganda, Dimmy Kanyankole, alisema ushirikiano huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa usafiri salama wakati unapohitajika zaidi.
“Kadri watu wanavyorejea kutoka mikoani na kuendelea na kazi na shughuli za kijamii, mahitaji ya usafiri yanaendelea kuwa makubwa. Ushirikiano wetu na SBL unalenga kufanya usafiri salama uwe rahisi, nafuu na unaopatikana kwa urahisi, ili kutoendesha gari baada ya kunywa pombe iwe chaguo rahisi zaidi.”
Kampeni hii inatekelezwa katika maeneo makuu ya burudani na maisha ya usiku jijini Dar es Salaam, huku mipango ikiendelea ya kuifikisha katika mikoa mingine nchini.
SBL na Bolt wanasisitiza kuwa Watanzania hawapaswi kuchagua kati ya kufurahia muda wa kijamii na kufika nyumbani salama. Kupitia mazoea chanya ya unywaji, kujali mwenzako na kutumia usafiri salama, Inawezekana Kabisa kufanya yote mawili.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com

  2. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  3. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button