Maandalizi Siku ya Kiswahili Comoro yaiva

BALOZI wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu amewahimiza wapenzi wa lugha ya Kiswahili nchini humo kujitokeza kwa wingi Jumapili wiki hii ili kukienzi Kiswahili katika hafla rasmi waliyoandaa kwenye ukumbi wa Bunge mjini Moroni.

Balozi Yakubu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa maandalizi yote ya maadhimisho hayo yamekamilika, ambapo Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja, Mohamed Mze atakuwa mgeni rasmi.

Amesema maadhimisho hayo ya Kiswahili nchini Comoro yatajumuisha burudani za Comoro na Tanzania, matokeo ya Shindano la Insha na pia kuona vyakula vya utamaduni wa Kiswahili ambapo wapishi mahsusi kutoka Tanzania watakuwepo.

Advertisement

Maadhimisho ya Kiswahili nchini Comoro yanatarajiwa kuhudhuriwa na wanafunzi, wataalamu wa Kiswahili na wadau kutoka mashirika ya kimataifa.

/* */