Madaktari kutoa huduma za kibingwa Shinyanga

SHINYANGA: Timu ya madaktari bingwa 36 wa magonjwa mbalimbali yakiwemo afya ya uzazi, figo na shinikizo la damu watakaotoa matibabu kwa wananchi wamewasili mkoani Shinyanga kwa lengo la kuwasogezea huduma za kibingwa karibu.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, alipowakaribisha wataalamu hao huku akieleza kuwa wananchi wamepata taarifa kuhusu ujio huo ambapo watasambazwa kwenye halmashauri zote sita na watatoa huduma kwa muda wa siku tano.
Mhita amesema ujio wa madaktari hao wananchi wataweza kupata elimu ya afya zaidi kwani bado baadhi ya wananchi wamekuwa na imani potofu wanapokuwa wamepatwa magonjwa hasa yasiyoambukizwa wanakwenda kwa waganga wa kienyeji kutibiwa kumbe yangehitaji madaktari bingwa na kupata kupona.
“Mkoa huu una halmashauri sita na wilaya tatu ambapo madaktari 1500 wa kutoka halmashauri zote kwa awamu iliyopita walipata mafunzo ya kitaalamu zaidi kutoka kwa nadaktari bingwa lengo wananchi wanapohitaji huduma za kibingwa angalau waweze kusaidiwa,”amesema Mhita.
Ofisa programu kutoka Wizara ya Afya Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto, Dk Michael Mbele amesema ni awamu ya nne sasa kuja shinyanga kupitia programu ya Madaktari bingwa wanaotoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa ikiwa na madhumuni ya kuwapunguzia gharama za matibabu na umbali mrefu wa kufuata matibabu.
“Kwa sasa awamu hii ya nne tunatarajia kuwafikia wagonjwa 30,000 lakini awamu iliyopita tuliwafikia takribani wagonjwa 240,000 na walipata huduma za kibingwa kwa gharama iliyo nafuu,”amesema Dk Mbele.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk Yudas Ndungile amesema wanafuraha kubwa kuwapokea madaktari waliokuja chini ya programu ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo wananchi watapata tiba za kibingwa bobozi na madaktari waliopo waliopo kwenye Halmashauri wataendelea kupata ujuzi zaidi.
“Ujio wa Madaktari hawa ni kurahisisha wananchi wa maeneo husika kupata matibabu karibu kwani waliowengi waliotakiwa kupata huduma za kibingwa walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugandao kupata matibabu hayo”amesema, DkNdungile.
Dk Ndungile amesema madaktari bingwa 36 waliowasili mkoani Shinyanga wanatarajiwa kusambazwa ikiwa kila halmashauri itaweza kupata madaktari 6 kwa ajili ya kutoa huduma kwa muda wa siku tano.
. I never thought I’d recover from the financial hit of my medical emergency—but this online method pays me $7,700 per month now. >>>> https://dailycash21.blogspot.com/