Madeni MSD yalipwe – RC Mwassa

KAGERA:  VITUO Vya kutolea huduma za afya vimetakiwa kuhakikisha vinalipa madeni wanayodaiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kabla ya mwaka wa fedha 2024/2025 haujaisha.

Akizungumza leo Juni 27, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Mstaafu, Hamis Mahiga amesema ili kujenga huduma madhubuti washirika wanapaswa kulipa madeni yao ili kupata huduma kwa wakati kutoka MSD.

Aidha, RC Mahiga ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Kagera na waganga wakuu wa wilaya na mkoa kuhakikisha wanatumia vyanzo vingine vya mapato kulipa madeni kwa wakati kwani wananchi wanaopata huduma za afya wapate huduma zote muhimu.

Amevitaka vituo vya afya kuhakikisha vinadhibiti mianya inayoweza  kupunguza mapato pamoja na watumishi wote kupata uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya kidigitali katika maswala ya kuagiza  dawa  unaolenga kuendana  na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

SOMA ZAIDI

“Lipeni madeni ya MSD izidi kuboresha hudum”

Mkurugenzi wa MSD Kanda ya Kagera,  Kalendelo Masatu akitoa mwenendo wa  huduma kwa wateja amesema serikali umetumia fedha  kuhakikisha vituo vinavyopata huduma za MSD vinapokea fedha ambapo Kanda ya Kagera MSD  inahudumia Mkoa wa Kagera na Geita katika vituo 413.

Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni  vituo vya afya kudaiwa ambapo Mkoa wa Kagera mpaka sasa unadaiwa zaidi ya Sh bilioni 3.2 na Mkoa wa Geita Sh bilioni 2.2.

Amesema vituo vinapaswa kulipa kwa wakati kwani ucheleweshaji wa fedha na mrundikano wa madeni unaweza kuathiri upatikanaji wa huduma kutoka katika bohari hiyo .

Alibainisha changamoto nyingine kuwa ni baaadhi kushindwa kutumia mfumo wa kidigital  katika maswala ya kuagiza mizigo ya dawa,kuagiza dawa bila kuzingatia mahitaji kamili, kutopeleka taaarifa kwa wakati na baadhi kushindwa Kuandika taarifa.

Amesema  MSD itaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha wanapata huduma bora pamoja na kujadili changamoto kwa pamoja Ili kuzitatua kwa msitakabari wa kuhakikisha Kila mwananchi anapata huduma kwa gharama nafuu

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema kuwa mkoa huo umepunguza deni kutoka Sh bilioni 6.3  zilizikuwa zinadaiwa na MSD hadi Sh bilioni 3.2 huku akidai kuwa mikakati iliyopo  kwa sasa ni kuhakikisha asilimia 50 ya mapato yote ya vituoni inaendelea kulipa deni hilo haraka ili kumaliza deni lote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button