Mafanikio Ilala yametokana na ushirikiano – Mpogolo

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema mafanikio ya wilaya hiyo yametokana na kufanya kazi kwa ushirikiano.
DC Mpogolo ametoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa katika hafla ya Ufunguzi wa Soko la Nyamachoma la Kumbilamoto katika hafla ya utiaji saini mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara, na kukabidhi gari la Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam.

Mpogolo amesema utendaji kazi wa pamoja na kuheshimiana katika wilaya unasaidia kujenga umoja na mshikamano na kuleta tija kwa kazi za serikali na kuwahudumia wananchi kwa manufaa ya maendeleo.
Katika hafla hiyo, Mpogolo, ametumia nafasi hiyo kumweleza Waziri Mchengerwa Ilala itaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza mapato ya ndani katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.

Aidha, ametoa ahadi ya kusimamia miradi yote ya maendeleo katika sekta mbalimbali ili iendane na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu suala la mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya jiji, Mpogolo ameeleza mikopo hiyo tayari imeanza kutolewa kwa mwananchi mmoja mmoja na vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu pamoja na kupatiwa elimu ili mikopo hiyo ikawe na faida kwa kuboresha biashara zao, kujikwamua kiuchumi na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine navyo vinufaike.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amempongeza Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya na Meya wa jiji hilo Omary Kumbilamoto kwa kuendelea kuwa viungo muhimu kwa wabunge na madiwani kuhakikisha Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezeka. hiyo kuendelea kusonga mbele kuwa ni kwa kufanya kazi kwa ushirikiano.



