MAGDALENA SHAURI: Aliyeweka rekodi mpya ya Taifa

MAGDALENA Shauri ni mmoja wa wanariadha wa Kimataifa wa kike wanaofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Amefanya maandalizi makubwa kujiandaa kwenda Tokyo, Japan lakini kwa bahati mbaya wanariadha wa kike wa Tanzania hawakwenda katika mashindano hayo.

SABABU ZA KUSHIRIKI

Wanariadha wote wa kike wa Tanzania hawakushiriki, licha ya maadalizi mazuri kwa sababu ya Riadha Tanzania (RT) kushindwa kuwapima wanariadha wake wa kike, ili kujua wingi wa homoni za kiume walizo nazo kama walivyoelekezwa na Riadha ya Dunia (WA).

SOMA: Mapokezi ya Magdalena yanoga Arusha

Wanariadha hao hawakushiriki na hilo lilitokea baada ya uongozi wa zamani wa RT kushindwa kutekeleza agizo hilo kwa wakati uliopangwa. Matamanio ya Magdalena yaliota mbawa na Gabriel Geay akienda mbio za Berlin Marathon iliyofanyika Ujerumani.

Alphonce Simbu alitwaa medali ya dhahabu katika mchezo wa mara thoni katika mashindano hayo ambayo hatujawahi kutwaa medali hio tangu kunzishwa kwa mashindano hayo mwaka 1986. Kubadili gia angani Magdalena baada ya kuona ameshindwa kushiriki mashindano ya dunia, akaamua kubadili gia angani na kuamua kwenda Chicago Marathon, mbio iliyofanyika huko New York, Marekani.

Huku alikimbia kwa usongo na kumaliza wa tatu kwa upande wa wanawake nyuma ya Waethiopia wawili, Hawi Feysa Gejia aliyetumia muda wa 2:14:56 na Megertu Alemu aliyetumia muda wa saa 2:17:18. Magdalena alitumia muda wa 2:18:03.

Mbio hizo kwa upande wa wanaume alishinda Mganda, Jacob Kiplimo kwa kutumia muda wa saa 2:02:23 na kupata ushindi wake wa kwanza katika marathoni kubwa. Akizungumza na mwandishi wa makala haya,  Magdalena anasema mbio hizo zilikuwa ngumu na Waethiopia hao wawili ndio walikuwa tishio kwake katika mbio za kuwania ubingwa huo.

Alijitahidi kukimbia na amebahatika kuweka muda wake bora binafsi lakini upinzani ulikuwa mkubwa pamoja na kujitahidi kupambana.

USHINDI WA SIMBU

Magdalena anasema kuwa ushindi wa Simbu, ambaye wanafanya naye mazoezi Pamoja chini ya kocha Mwingereza ulimtia nguvu na ari kubwa ya kufanya vizuri Chicago Marathon 2025.

Siku chache zilizopita, Simbu alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya riadha ya dunia huko Tokyo, Japan, ikiwa ni Mtanzania wa kwanza kupata dhahabu katika mashindano hayo.

MIPANGO YA BAADAE

Mipango yake ya baadae ni kushiriki mashindano makubwa ili kuboresha kiwango chake siku hadi siku na kufanya vizuri zaidi katika riadha.

WITO KWA CHIPUKIZI

Magdalena anasema wanariadha chipukizi wajitume na wafanye mazoezi kwa bidii bila kusahau nidhamu. “Lazima wawe na nidhamu ya kila kitu, kujituma kufanya mazoezi na kuwa na nidhamu kwa ujumla,” anasema.

ALIKOTOKEA MAGDALENA

Alizaliwa miaka 29 iliyopita na kuanza kukimbia mbio za kati na kupanda taratibu hadi kuwa mwamba wa mbio za meta 5,000 na 10,000, hadi kuwa bingwa wa taifa.

Baada ya kutamba kwa muda katika mbio za meta 5,000 na 10,000 akahamia katika mbio za barabarani za kilometa 10 barabarani na zile za marathoni na kumfanya kupata uzoefu wa mbio hizo ndefu, tofauti na wanariadha wengi wanaokimbilia moja kwa moja marathoni.

Mbali na marathoni, amekimbia mbio za nyika za umbali tofauti na kumfanya kuwa na uzoefu wa mbio hizo ndefu tofauti na wanariadha wengi, ambao huanzia moja kwa moja katika mbio ndefu.

MASHINDANO ALIYOSHIRIKI
Magdalena ameshiriki mashindano mbalimbali kama vile yale ya riadha ya dunia, mbio za nyika za dunia,

Michezo ya Olimpiki mwaka 2024 na kushika nafasi ya 40, Paris, Ufaransa. Pia, Magdalena amewahi kushiriki mbio za nusu marathoni.

REKODI YA TANZANIA

Magdalena amekuwa akishikilia rekodi ya Tanzania katika nafasi ya tatu, nyuma ya Tigst Assefa aliyevunja rekodi ya dunia kwa muda 2:11:53.

Kwa hiyo, Magdalena ameweka muda bora mpya na kuweka rekodi mpya ya Tanzania ya muda wa 2:18:03 na kuipita ile ya zamani kwa sekunde 38. Rekodi ya zamani ilikuwa saa 2:18:41.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button