Magereza Shinyanga wakabidhiwa majiko ya gesi

SHINYANGA: JESHI la Magereza mkoani Shinyanga limepokea mitungi ya gesi na majiko 221 kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani huku wakitakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza nishati hiyo nakuondokana na matumizi ya kuni yanayoleta uhalibifu wa mazingira.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) injinia Ahmed Chinemba amesema hayo leo wakati wa kukabidhi mitungi hiyo kwa maofisa wa Jeshi la Magereza Mkoa huku akieleza mkataba wa utoaji ruzuku kwenye mitungi hiyo ulisainiwa mwaka 2024 mwezi Septemba, ukiwa na gharama ya Sh bilioni 35.2.
Chinemba amesema maofisa wa magereza wanatakiwa kuwa mabalozi katika utumiaji wa gesi kwani bado taassi zingine na wananchi maeneo ya vijijini wanakata miti hovyo kwa matumizi ya nishati ya kuni ambayo hivi sasa inazuiliwa kwa kupelekea kuhalibu mazingira.
“Ninawapongeza Jeshi la Magereza wamekuwa vinara kwa utumiaji wa gesi hasa kwenye magereza ukilinganisha na taasisi zingine kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alitoa agizo kwenye taasisi zenye watu zaidi ya 100 ni lazima watumie gesi sio kuni,”amesema Chinemba.
Chinemba amesema mradi huu Wakala wa Nishati Vijijini ulitoa Sh Bilioni 26 na Jeshi la Magereza limetoa Sh bilioni 4 hivyo kunaushirikiano unaotumia mfumo mmoja ambapo unalenga kupunguza gharama za matumizi ya nishati safi katika Mageregeza yote nchini na malengo kufikia mwaka 2034 matumizi ya gesi yawe asilimia 80.
Dk Joseph Sambali kutoka dawati la Jinsia Wakala wa Nishati Vijijini alisema mradi utakuwepo kwa muda wa miaka mitatu unahusisha usambazaji wa majiko ya gesi na mitungi 15,126 na usambazaji wa makaa ya mawe tani 850, majiko banifu 344 kwa kambi za magereza nchini na mashine 61 za kuzalisha mkaa mbadala.
“Kwa mkoa wa Shinyanga nao umefaidika kupata mitungi ya gesi yenye ujazo wa kilo 15 kwa watumishi wote na tayari imekuwa kwenye usambazaji wa mkaa mbadala unaotekelezwa na kampuni ya Stamico kwa Magereza ya Shinyanga na Kahama wote wamepata tani tano tano na majiko banifu matatu matatu mpaka sasa”amesema Dk Sambuli.
Mkuu wa Gereza Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi hilo Nobert Ntacho amesema wanaishukuru serikali na kukiri kupokea mitungi ya gesi ambayo familia zao na wafungwa wanakwenda kunufaika kwa wilaya ya Kahama na Shinyanga ambapo tayari wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa nishati hiyo yenye usalama zaidi.
Mkuu wa Gereza Wilaya ya Shinyanga Kamishina Msaidizi wa jeshi la Magereza Martin Kunambi amesema gereza lina wahalifu na wafungwa 263 ambapo walianza kubadilika kwa mfumo wa upikaji kwa matumizi ya kuni tangu agizo la Rais Samia Suluhu Hassani kueleza taasisi yenye watu zaidi ya 100 waanze kutumia gesi na kuachana na matumizi ya kuni.
“Tunaipongeza na kuishukuru serikali tumepokea mitungi hii ya gesi ipatayo 221 sawa na idadi ya askari na watumishi waliopo na tunaendelea kutumia makaa yam awe na gesi na hata majiko yetu tumeyab