Kabila akabiliwa na hukumu ya kifo

DR CONGO : WAENDESHA Mashtaka wa Kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameiomba Mahakama ya Kijeshi kutoa hukumu ya kifo kwa Rais wa zamani, Joseph Kabila, kwa tuhuma za uhaini na kushirikiana na kundi la waasi la M23/AFC.

Kabila anadaiwa kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu pamoja na njama za kutaka kupindua serikali kupitia ushirikiano wake na vuguvugu la M23. Katika kikao cha kusikiliza kesi hiyo kilichofanyika mjini Kinshasa wiki iliyopita, upande wa mashtaka uliwasilisha pia ombi la kutaifishwa kwa mali za kiongozi huyo wa zamani.

Hata hivyo, Kabila hakuhudhuria mahakamani wakati ombi hilo likiwasilishwa na mpaka sasa hajatoa tamko rasmi kwa umma. Aidha, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) Jumamosi, Kabila aliandika ujumbe unaoashiria msimamo wake. SOMA: M23 Yatuhumiwa Kuua 169 DRC

“Iwe Mashariki au Magharibi haitaweza kutugeuza kutoka njia yetu. Watu wa Congo hawatavumilia tena udikteta au udhalimu unaochochewa na tamaa. Mwisho wako tayari umeandikwa, kama jua linalotua kila jioni. Mapenzi ya watu wenye msimamo thabiti yana nguvu kuliko nguvu zote kwa pamoja.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button