Majaliwa alipongeza bunge kupitisha bajeti

DODOMA — Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza wabunge kwa kupitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026 kwa asilimia 98.7, akisema ni ishara ya uzalendo na imani kwa serikali ya awamu ya sita.
Amesema mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano mkubwa miongoni mwa wabunge, ambapo michango yao ilitoa dira sahihi ya kisera kwa maendeleo ya wananchi. Aliongeza kuwa kila mbunge alionesha dhahiri kujali mustakabali wa taifa.
SOMA ZAIDI
Majaliwa pia aliwapongeza kwa kazi waliyoifanya tarehe 24 Juni, 2025, aliposema: “Hakika ninyi ni wazalendo, mmevunja rekodi, mnaipenda nchi yenu na mnathamini kazi kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan.”
Aliwataka wabunge kurudi majimboni kuwa mabalozi wa utekelezaji wa bajeti hiyo na kuwaeleza wananchi kuhusu fursa zilizomo. Alisema dira ya maendeleo ya 2025-2050 itakuwa mwongozo wa taifa.
Waziri Mkuu amesema kuwa mchango wa Bunge umebeba uzito mkubwa katika mwelekeo wa serikali ijayo na maendeleo ya taifa