Majaliwa amwakilisha Rais Samia kongamano la Tehama

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la Tehama linalofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2024.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda  ya maonesho kwenye kongamano hilo, Waziri Mkuu  ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa sekta ya Tehama.

Advertisement

Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya uwekezaji unaofanya na serikali katika sekta ya Tehama ili kukuza uchimi binafsi na taifa kwa ujumla.

Kaulimbinu ya kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii”.