Makandarasi wanawake wapewa mradi wa bil 42/-

SONGWE: MAKANDARASI wanawake wazawa wakabidhiwa mradi wa km 20 ujenzi barabara kiwango cha lami kutoka kata  ya Luanda hadi Idiwili wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiwa ni mwendelezo mpaka katika Mji wa Itumba km 79 wilaya ya Ileje kuunganisha na nchi jirani ya Malawi.

Akiwakabidhi makandarasi wanne wanawake ambao wataanza ujenzi wa barabara hiyo ya Luanda, Lyula mpaka Idiwili kwa kiwango cha lami kuanzia mwezi September, Meneja wa Tanroad Mkoa wa Songwe Injinia Selemani Bishanga amesema ujenzi wa barabara hiyo ni mwendelezo mpaka kata za Hezya mpaka kata ya Itumba ikiunganisha na nchi jirani ya Malawi.

Amesema mradi huo wa awali ujenzi  km 20 kutoka Luanda mpaka Idiwili utajengwa kwa gharama ya Sh bilioni 42 ambapo unategemewa kukamilika mwezi September, 2026.

“Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa mkoa wa Songwe, ambapo kuna miradi miwili yenye thamani ya shilingi bilioni 124 tayari imekamilika ukiwepo mradi wa km 50 barabara kutoka Mpemba mpaka Isongole wenye thamani ya Sh bilioni 107 na ujenzi wa daraja mita 84 linalounganisha mkoa wa Songwe na Rukwa lenye thamani ya Sh bilioni 17” amesema Bishanga

Amesema wanawake wazawa wamepata mradi huo mkubwa kutokana na mabadiliko kidogo ya Sheria ya manunuzi ambayo Rais wa awamu ya sita ameyafanya kuhusisha wanawake, walemavu, vijana na wazee kushiriki kupata fursa kubwa  katika ujenzi wa miradi mbambali mikubwa.

Kwa upande wake Rais wa chama cha makandarasi wanawake Tanzania Judith Odunga amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mabadiliko ya sheria ya manunuzi ambapo wakandarasi wanawake wameanza kunufauka na miradi mikubwa ya kimkakati.

“Kutoka miradi ya Sh bilioni 10 tuliyokuwa tunafanya, kutokana na mabadiliko kidogo aliyofanya Rais Samia hivi sasa tuna uwezo wa kufanya miradi yenye thamani mpaka Sh bilioni 50,

Kwa mradi huu wa km 20 Luanda , Iyula mpaka Idiwili tutautekeleza kwa nguvu zote na kwa ubora mkubwa , huku tukiwapa fursa wanawake wenzetu wa kata na vijiji jirani wa kazi mbalimbali za usaidizi,” amesema Odunga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button