Makete kupata nyasi za mifugo kama za Brazil

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimedhamiria kuanzisha shamba la nyasi lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 20,000 kwa ajili ya kulisha mifugo eneo la Makete.
Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amesema hayo katika mikutano ya kampeni iliyofanyika Wanging’ombe na kwenye Viwanja vya Mabehewani mjini Makete mkoani Njombe.
Dk Nchimbi amesema shamba hilo litapandwa nyasi ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikisifika nchini Brazil kwa ubora wake katika kulisha ng’ombe.
Pia, amesema CCM imeweka mkakati wa kuendeleza zao la parachichi kwa kusambaza mbegu na miche bora ya zao hilo kupitia vitalu vya miche na kuboresha huduma za ugani.
SOMA: Chongolo: Nchimbi ni chaguo sahihi
Dk Nchimbi amesema visima 150 vya umwagiliaji vitachimbwa, sambamba na ujenzi wa mabwawa ya maji ili kuongeza tija ya kilimo.
Amesema CCM ikiwa madarakani, itahakikisha ruzuku kwa wakulima inaongezwa na kusimamiwa, ikiwemo ya mbegu, mbolea na chanjo za mifugo.
Dk Nchimbi ameisema miongoni mwa miradi mikubwa itakayotekelezwa Makete ni wa umwagiliaji kwa njia ya mifereji kilometa 50 ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Pia, amesema katika miaka mitano ijayo serikali ya CCM itaweka kipaumbele kwenye ujenzi wa viwanda vya kusindika na kuchakata mazao ya kilimo, ikiwemo parachichi na mahindi ili kupunguza upotevu wa mazao na kutoa ajira kwa vijana.
“CCM ikiahidi inatekeleza, tutahakikisha viwanda hivi vinajengwa na kuimarishwa, ili wakulima wasipate hasara na vijana wapate ajira,” amesema Dk Nchimbi.
Ameahidi kukamilisha miradi ya maji katika vitongoji vyote vilivyobaki Makete na Wanging’ombe sanjari na ujenzi wa matanki na mtandao wa mabomba.
Dk Nchimbi amesema vijiji vyote vilivyobaki vitapatiwa umeme na ujenzi wa njia kuu ya umeme kutoka Makambako kwenda Makete utapewa kipaumbele.
Amesema Hospitali ya Wilaya ya Makete na ya Wanging’ombe zitaboreshwa kwa kuongezewa majengo, vifaa tiba na watumishi na pia vituo vipya vitatu vya afya na zahanati zaidi ya 20 vitakamilishwa.
Dk Nchimbi amesema yatajengwa madarasa mapya 168 katika shule za msingi na madarasa 60 katika shule za sekondari na pia zitajengwa shule mpya tano za msingi.
Amesema barabara za Makete–Mbeya, Sonje–Kikondo kilometa 96, Kitulo–Iliho kilometa 36, Ndulamo–Kitulo
kilometa 42, Kitulo–Chimala kilometa 41 na Matamba– Mfumbi kilometa 33, Njombe–Iyaga kilometa 74
zitakamilishwa.
Dk Nchimbi amesema vijiji vyote vilivyobaki vitapatiwa umeme na ujenzi wa njia kuu ya umeme kutoka Makambako kwenda Makete utapewa kipaumbele. 威而鋼價格
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Join this online home job right now and start making more than $500 every single day. It’s easy work—if you know how to use Facebook, then this job is for you. No boss watching over you, and you can work whenever you want from home. I made $18,632 last month by doing this just 2 hours a day after college. Curious to know more or join? Just visit this website for details.
COPY THIS →→→→ http://Www.Cashprofit7.site
i amesema vijiji vyote vilivyobaki vitapatiwa umeme na ujenzi wa njia kuu ya umeme kutoka Makambako kwenda Makete utape 犀利士ptt
i amesema vijiji vyote vilivyobaki vitapatiwa umeme na ujenzi wa njia kuu ya umeme kutoka Makambako kwenda Makete 必利吉ptt