Makonda asisitiza amani muda wote

ARUSHA: MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ya nchi ili taifa liwe salama wakati wote.

Makonda alisema hayo Oktoba 27, wakati akizungumza kwenye ibada ya Kanisa la Calvary Temple lililopo Mtaa wa Kilombero Arusha.

“Amani ya nchi hii haipo kwenye bunduki wala waganga wa kienyeji au elimu tulizonazo,amani ya taifa ipo mikononi mwa watumishi wa Mungu, amani ya taifa letu likitoeka watu wa kwanza kuhojiwa ni watumishi Mungu mkikubali amani hii ikatoeka tutapata tabu sana,” alisema Makonda.

Aliwasihi viongozi wa dini kuwa viongozi wa amani ya nchi kwa kuwa wanasiasa na viongozi wengine wanapaswa kuwakimbilia watumishi wa Mungu hivyo haipaswi viongozi wa dini wawakimbilie viongozi wa siasa kwa sababu kwa viongozi wa dini kuna usalama.

Aliwaomba waumini wa kanisa hilo kutochoka kuliombea taifa na viongozi wanaohuduma katika nafasi mbalimbali kwa kufanya hivyo watakuwa sehemu ya uongozi na maamuzi yao ya kuongoza katika nafasi walizonazo.

“Kiongozi hatoki mbinguni anazaliwa anabeba, analelewa,anafundishwa, anatengenezwa na ikifika mahala anasimama mwenyewe na ukimpata kiongozi anayetoka kwenye kinywa cha Mungu akisimama mahali popote anatengeneza utofauti kati ya giza na nuru,”alisema.

Aliongeza “Ninauhakika nitashinda ubunge kwa kuwa nina uhakika naomba msiniache katika kushiriki nafasi za uinjilishaji kwa sababu zipo nyakati nitaongozana nanyi.Ningewaomba mnibebe kwenye maombi msinibebe kwenye kura ningependa zaidi niombewe ili nikatimize kusudi la Mungu ili nikishinda nikikaa kwenye kile kiti niwe nimeketishwa kwa maombi ya watakatifu na waumini wa Mungu,”.

Makonda alisema anatamani kuona watoto wadogo wanafundishwa na wanalijua neno la Mungu na wanaishi katika maadili na misingi ya Mungu ili kupunguza matukio ya kikatili kwa sababu watu watakuwa wamejengwa kwenye imani ya Mungu tangu wakiwa watoto.

Alisema wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa huo alipotembelea shule aliwauliza waalimu kama wanafunzi wanasoma somo la dini lakini alijibiwa kwa waalimu wa dini hawafiki kwenye shule kufundisha neno la Mungu.

Makonda alisema akiingia madarakani anatamani jimbo hilo kuwa na mashindano ya kusoma biblia ili kuongeza imani kwa watoto.

“Kulikuwa na ajari katika mkoa huu lakini tuliona hakuna namna zaidi ya kumuomba Mungu na hatukuongeza trafiki wala kamera bali tuliita jina la Mungu tena hadharani na Mungu akatusikia,” alisema.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button