Makonda kuifanya Arusha kitovu cha uchumi

ARUSHA: MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Paul Makonda ameeleza kuwa akiingia bungeni atahakikisha mkoa huo unakuwa kitovu cha uchumi nchini.

Amesema ataimarisha uwekezaji kwenye viwanda, miundombinu, huduma bora kwa wananchi na ujenzi wa mazingira rafiki ya kiuchumi. Makonda alisema hayo jana akiwa mtaa wa Unga limited wakati akifanya ziara ya mtaa kwa mtaa kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi.

“Eneo la viwanda ndilo linalotoa fursa kubwa ya ajira na kuinua kipato cha wananchi,eneo la pili lenye umuhimu mkubwa ni miundombinu, ikiwemo maji, shule, afya, barabara na kumbi mbalimbali kwa sababu ujenzi wa miundombinu imara ni nguzo ya maendeleo na ndio msingi wa uchumi endelevu,”alisema Makonda.

Alieleza kuwa atahakikisha serikali inajenga kumbi za mikutano na maeneo ya uwekezaji ambayo yote yanalenga kuleta wageni ili kuongeza mzunguko wa fedha na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Arusha kama ilivyofanya serikali ya Awamu ya Sita kujenga viwanja vya mpira kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

“Juzi nilikwenda kuangalia bandari ya Dar es Salaam, Rais Samia amewekeza kwa kiwango kikubwa. Tumeona mizigo ikiongezeka kutoka tani milioni 18 hadi milioni 27 kwa mwaka. Sio tu bandari ya Dar es Salaam, bali pia Mtwara imeongezeka kutoka tani 590,000 hadi milioni 2.59, na Tanga kutoka tani 830,000 hadi milioni 1.3. Hii inaonesha namna uwekezaji unavyoweza kukuza uchumi,” alisema.

Alisema ataweka mkazo katika kuboresha huduma kwa wananchi kwa kuzingatia kaulimbiu ya mgombea urais wa CCM, “Kazi na Utu” inayolenga kujenga uchumi na kuboresha mazingira, lakini utu ni kumthamini kila mtu kwa heshima bila kujali kipato chake.

Aliahidi kusimamia upatikanaji wa haki za wananchi wa jimbo hilo kuanzia hospitali,serikali za mitaa,vituo vya polisi na sehemu zote zinazotolewa huduma za kijamii.

“Hatutambagua mtu. Tutahakikisha kila mmoja anaheshimika, anapata haki yake na kutimiza wajibu wake katika uongozi wangu hakuna mwanamke atakayenyanyaswa hiyo ndiyo ndoto yetu,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa ajili ya kumchagua kiongozi mwenye uwezo, busara na uzoefu wa kulinda uchumi, diplomasia na usalama wa nchi kama alivyoonyesha Rais Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button