Makundi maalumu kupewa kipaumbele upigaji kura

MANYARA: Makundi maalumu ya wazee, wajawazito na watu wenye mahitaji maalumu yamesisitizwa kupewa  kipaumbele katika zoezi la kupiga kura linaloendeleo katika  vituo vya kupigia kura ili kutoa haki ya kushiriki uchaguzi Mkuu kwa watu wote.

‎Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Almish Hazal wakati akipiga kura katika kituo cha kupigia  kura cha Shule ya Msingi Bomani wilayani humo.

‎Amesema makundi hayo ni muhimu kusaidiwa na kuhudumiwa mapema na kuhakikisha yanaondoka katika vituo vya kupigia kura.

‎Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Hanang mkoani Manyara, Geogrey Abayo amesema pale ambapo makundi hayo yanafika kwenye kituo cha kupigia kura ili waweze kupiga kura mapema na kuondoka kurudi nyumbani wasimamizi wa vituo ni muhimu wakawasaidia.

‎Ameema hayo katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Manangararay kilichopo katika kata ya Katesh Wilaya ya Hanang kwamba ni muhimu watu hao wakapiga kura mapema na kuondoka pasipo kufanya foleni ya watu wote

‎Amebainisha kuwa jumla ya kata 33 zilizopo wilayani humo idadi ya wanaotarajiwa kupiga kura katika vituo vya uchaguzi 506 ni 196,665 na kwamba vifaa vyote muhimu kwa ajili ya zoezi la upigaji kura ikiwemo masanduku ya kura  vimekamilika na kwamba hakuna mapungufu yaliyojitokeza.

‎Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda katika vituo mbalimbali vya kupiga kura ili kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi kwani hakuna msongamano wa watu.

‎”Hawatachelewa kwasababu tumejipanga vizuri na kila kituo kina idadi ya watu ambao ukifika tu unapiga kura na kuondoka kwenda nyumbani,” amesema Abayo.

‎Sheikh Mkuu Wilaya ya Hanang, Sheikh Muh’di Tonka amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura mapema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button