Mutharika aongoza asilimia 66 ya kura

MALAWI : RAIS wa zamani wa Malawi, Peter Mutharika, anaendelea kuongoza dhidi ya mpinzani wake, rais aliyeko madarakani Lazarus Chakwera, katika uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16. Kwa mujibu wa matokeo ya awali kutoka theluthi mbili ya mabaraza ya uchaguzi, Mutharika anaongoza kwa asilimia 66 ya kura halali.

Chakwera, ambaye anatafuta kuchaguliwa kwa mara ya pili, amepata asilimia 24 pekee ya kura, hali inayomuweka katika nafasi ngumu. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, mgombea atatangazwa mshindi moja kwa moja endapo atapata zaidi ya asilimia 51 ya kura zote. SOMA: MCP yadai kuibiwa kura uchaguzi Malawi

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema Mutharika, mwenye umri wa miaka 85, ameonesha upinzani mkali licha ya kustaafu siasa baada ya kushindwa mwaka 2020. Endapo hakuna mshindi wa moja kwa moja, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button