Mali, Burkina Faso wasusia kikao cha ulinzi

NIGERIA : BURKINA Faso na Mali zimegoma kupeleka  wawakilishi wake katika mkutano wa kijeshi wa bara la Afrika unaoendelea jijini Abuja, Nigeria. Mataifa hayo mawili yanayoongozwa na tawala za kijeshi yameendelea kuwa na uhusiano mbaya na majirani zao katika kanda ya Afrika Magharibi, hali iliyotajwa kuwa chanzo cha msimamo wao.

Mkutano huo umewakutanisha wakuu wa majeshi na maafisa waandamizi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, ukiwa na ajenda kuu ya kujadili mikakati ya pamoja ya kiulinzi na namna ya kushughulikia changamoto za usalama barani. SOMA: NIGERIA: Hatma ya Burkina Faso, Mali na Niger kujulikana kesho

Aidha, mjadala umeelezwa kulenga pia katika kuimarisha mshikamano wa kijeshi baina ya nchi wanachama, ili kuendeleza juhudi za kudhibiti vitisho vya kigaidi na mizozo ya kikanda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button