Malori 16 ya misaada yateketea Sudan

DARFUR: UMOJA wa Mataifa umesema shambulizi la droni limesababisha kuungua kwa malori 16 ya misaada ya chakula katika eneo la Darfur Kaskazini, Sudan.
Tukio hilo limeathiri juhudi za kufikisha msaada katika eneo linalokabiliwa na njaa kali. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Daniela Gross, alisema madereva na maafisa wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) waliokuwa kwenye msafara huo wako salama.
Hata hivyo, haijulikani kundi lililohusika na shambulizi hilo la pili katika miezi mitatu. Mapema Juni, msafara wa WFP na UNICEF pia ulishambuliwa karibu na mji wa El-Fasher na kusababisha vifo vya watu watano.
Umoja wa Mataifa umesema mashambulizi haya yameathiri pakubwa ugawaji wa misaada muhimu. SOMA: Malori 120 ya msaada yaingia Gaza