Mama wa watoto 13 asimulia machungu mlo mmoja

FAMILIA yenye watoto 13 ya Neema Kenge ( 39), na mumewe Simon Zongo, inayoishi mtaa wa Mgonahazeru kata ya Mbuyuni, Manispaa ya Morogoro ikikabiliwa na changamoto ya malezi ya watoto hao kati ya 15 waliowazaa kutokana na ugumu wa maisha unaochangiwa na kipato duni .

Mama huyo amekiri kuwazaa watoto 15 kati yao wawili walifariki dunia wakiwa wadogo na hivyo kuwa na watoto 13 akiwemo mchanga wa mwezi mmoja na wiki mbili.

Kati ya watoto aliowazaa wakike ni tisa na wakiume ni sita wote na amewazaa na mume wake huyo .

Anasema kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu ya ukosefu wa chakula kwa familia yake kwani wanalazimika kula mmlo mmoja ama wiwili isiyojitosheleza, ukosefu wa huduma za afya , na malazi kwa kujibanza kwenye vyumba wiwili .

Neema anasema wanakaa kwenye nyumba ya familia ya mumewe ambayo ina watu wengine na ipo kwenye mazingira hatarishi.

Amesema ya kwamba mwanae wa kwanza alimzaa mwaka 2000, wapili mwaka 2002 , watatu mwaka 2004 , wanne mwaka 2005 , watano mwaka 2007 , mtoto wa sita mwaka 2009 , mtoto was aba mwaka 2011 , mtoto wa nane mwaka 20013 , mtoto mwingine wa 13 alizaliwa mwaka 2021 na mtoto wa 15 amezaliwa mwaka 2024 akiwa na umri wa mwezi moja na wiki mbili.

Neema amesema watoto wake wawili ambao ni mzao wa tisa na wa 14 walifadiki dunia wakiwa wadogo na kutokana na mateso ya maisha magumu hatarajii tena kuzaa.

“ Maisha ninayoyapitia ni magumu mimi na watoto wangu kwani analala na watoto watano chumba kimoja na wengine chumba cha pili , baba yao mara nyingi halali nyumbani kutokana na majukumu yake” amesema Neema.

Licha ya kushindwa kuelezea kwa kina kufuata uzazi wa mpango pamoja na kujaribu dawa alizikuwa akitumia zilikuwa kikimdhuru na hivyo kulazimika kuendelea kuzaa watoto .

“ Dawa za uzazi wa mpango nikitumia zinadhuru hivyo niliona niendelea kuzaa hadi uzazi utakapoisha ..lakini kutokana na mateso haya siwezi tena kuendelea kuzaa “ anasema Neema.

Hivyo alitumia fursa hiyo kuomba msaada kutoka kwa wadau kumsaidia kimaisha kwani kutokana na changamoto zinazozipata zinachangia hawa watoto wake kushidwa kuhudhurua vyema masomo shuleni.

Kutokana na kukuswa kwa changamoto anazozipitia Waandishi wa habari pamoja na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Polisi Wilaya ya Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pendo Meshurie walijichangisha na kupata fedha kidogo na kumkabidhi kwa siku ya Februari 2, 2024 ili ziweza kumsaidia kupata chakula kwa siku hiyo .

Habari Zifananazo

Back to top button