Mambo safi barabara Biharamulo

KAGERA: Wananchi wa Mji wa Biharamulo wataondokana na changamoto ya vyombo vya moto  kuharibika baada ya wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuendelea kuunganisha barabara za Biharamulo Mjini kwa kiwango cha lami.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Biharamulo, Masuka Lung’wecha ametoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Biharamulo Mjini mbele ya Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ussi. Barabara hiyo ya kilometa 0.6 imegharimu Sh milioni 306.9.

“Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru barabara hii ilikuwa hatarishi hasa nyakati za mvua hasa kuharibika kwa vyombo vya moto kama piki piki na magari ,lakini pia  wananchi walipata adha ya vumbi na matope na sasa TARURA imeongeza hadhi katika mji huu kwa kujenga Barabara ya mjini kwa kiwango cha lami,”amesema Lung’wecha.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi amewapongeza TARURA kwa kutekeleza miradi kwa weledi na viwango hasa kungarisha makao makuu ya wilaya ya Biharamulo kwa kuendelea kuweka lami katika barabara za Wilaya za Biharamulo.

Ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Biharamulo kutumia fursa ya uwepo wa barabara hiyo kufanya biashara usiku na mchana na kuongeza juhudi za uwekezaji ,kujenga Nyumba za wageni na kungarisha nyumba zao kwani tayari kuna lami

Mradi huo umefikia asilimia 90 ambapo kukamilika kwa mradi huo kunaifanya halmashauri ya mji wa Biharamulo kuongeza mtandao wa lami katika Barabara zinazozunguka ofisi za halmashauri hiyo.

Mwenge wa uhuru umemaliza mbio zake mkoani Kagera ambapo miradi ya Barabara zinazohudumiwa na TARURA iliyokaguliwa kutembelewa kufunguliwa na kuwekewa mawe ya Msingi ilikuwa 6 na Daraja moja .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button