Manyara yapamba moto mapokezi ya Dk Samia

MANYARA: Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu Hassan katika  Mkoa wa Manyara yamepamba Moto ambapo wananchi wengi kutoka wilaya zote za Simanjiro, Kiteto,Mbulu,Hanang na Babati wamewasili mji wa Babati.

‎Wakizungumza katika shamrashamra za kumpokea kiongozi huyo wananchi hao wamesema wameanza maandalizi ya kumpokea kiongozi huyo kutokana na kazi kubwa ya maendeleo ambayo ameyafanya ikiwemo ujenzi wa nyumba za waathiriwa wa maporomoko ya mawe na udongo yaliyotokea wilaya ya Hanang.



‎Nao baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara,akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa, katibu wa  CCM Mkoa na Katibu Mwenezi wa Mkoa, wamesema maandalizi yamekamilika ya kumpokea kiongozi huyo ambapo wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 4 katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati kusikiliza sera za chama hicho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button