Maofisa habari watakiwa kuhamasisha amani EAC

MAOFISA uhusiano kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameagizwa kutangaza zaidi habari zinazohusu jumuiya hiyo katika kukuza uchumi, soko la pamoja, miundombinu ya barabara pamoja na kuhamasisha amani na maendeleo yanakua katika nchi hizo za jumuiya.

Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva wakati wa ufunguzi wa mkutano Wiki ya Mahusiano ya Umma ya Afrika Mashariki (EAPRW).

Vilevile, kulifanyika uzinduzi wa ofisi ya umoja huo jijini Arusha chini ya Kaulimbiu, ”Kuimarisha Uaminifu Kati ya Serikali na Wananchi Katika Afrika Mashariki, Nafasi ya Kimkakati ya Mahusiano ya Umma”.

Alisema kila nchi ndani ya EAC ina habari zinazopaswa kuandikwa na jamii ijue mambo yanayofanyika. Kupitia umoja huo, maofisa hao wana jukumu za kuandika na kutangaza.

“Lazima muwe simulizi juu ya mambo mbalimbali yanayofanywa na EAC, pia kufunguliwa kwa ofisi hii ni hatua muhimu kikanda ya kukuza na kuendeleza ubora wa mawasiliano na utafiti zaidi,” alisema.

Waziri wa Mawasiliano na Habari wa Burundi, Gabby Bugaga alisisitiza kuimarisha zaidi uhusiano, kukuza amani na kujenga uaminifu kati ya serikali na wananchi, ikiwemo kutetea ukweli.

“Lazima tuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, kukuza amani, kuelimisha jamii na kuendeleza mazungumzo ya msingi na maelewano kwa pande zote,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla alisema maofisa hao wana jukumu la kuimarisha imani ya umma kwa taasisi, kusimamia masuala kwa ubora unaolingana na majukumu yao.

Alisema pia wanapaswa kuunda simulizi za kitaifa na kikanda, kujenga uelewa katika jamii mbalimbali za mawasiliano na kuunga mkono ujumuishaji wa kikanda kupitia mawasiliano yenye taarifa sahihi.

Ronald Matunga ambaye ni Ofisa Habari kutoka Uganda alisema jumuiya hiyo imeundwa ili kuwaleta kwa pamoja maofisa hao wajifunze kwa pamoja, washirikiane na kuinua viwango vya taaluma, ikiwemo uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Mahusiano ya Umma Afrika Mashariki.

Wakati huo huo, Rais wa Chama cha Maofisa Uhusiano kutoka Tanzania, Assah Mwambene alisema ofisi hiyo itatumika kama kitovu cha maendeleo ya kitaaluma, ubadilishanaji wa maarifa na kukuza viwango vya kikanda.

Pia, ni injini ya mawazo, utafiti, ushirikiano na mustakabali wa mawasiliano.

Aliwasihi maofisa hao kuhakikisha wanapata watafsiri wa sera, uwazi, walinzi wa taarifa sahihi na wawezeshaji wa ushirikiano wenye maana kwa wananchi na wanahabari.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button