Maoni:Tunawatakia Ramadhani njema Waislamu

WAISLAMU wameanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Sehemu kubwa ya waumini wa dini hii walianza jana. Hiki ni kipindi ambacho hufanya ibada zaidi na kujiepusha na matendo maovu.
Kulingana na kalenda ya Kiislamu, Ramadhani ni mwezi wa tisa na Waislamu duniani kote huutukuza kwa kufunga na kufanya ibada.
Hiki ni kipindi cha baraka, tafakari na kujitolea kwa ajili ya ibada ambacho waumini wanategemewa kujitenga na mambo yasiyokuwa ya maana ili waweze kuimarisha uhusiano wao na Mwenyezi Mungu.
Ni muhimu kwa kila muumini kutafakari juu ya maana halisi ya kufunga, ambayo ni kujifunza uvumilivu, kutoa na kuimarisha ushirikiano.
Tunasisitiza Waislamu kuzingatia mawaidha ambayo yamekuwa yakitolewa mara nyingi yakielimisha kwamba Ramadhani si tu kipindi cha kufunga kula na kunywa bali pia ni muda wa kuzingatia matendo mema.
Kipindi cha mfungo ni cha kujiepusha na maneno mabaya, hasira na ubinafsi. Wanaofunga wawe mfano mzuri wa maadili mema kwa wengine.
Kiwe kipindi cha kuonesha zaidi huruma kwa wahitaji, kusaidia wanaopitia changamoto za kiuchumi na kutoa kwa wingi kwa ajili ya kufanya mema.
Kila muumini aliyefunga atambue kwamba ibada haitakamilika bila matendo ya huruma na ushirikiano. Ramadhani iwe fursa ya kubadili tabia, kuwajali wengine katika jamii, kuimarisha ushirikiano, amani na utulivu.
Wakati tukihimiza Waislamu kutekeleza kwa vitendo mfungo, kwa upande mwingine jamii pia haina budi kuwaunga mkono uwe wa amani na utulivu.
Hii ni pamoja na wafanyabiashara kuepuka kupandisha bei za bidhaa hususani vyakula vinavyotegemewa na waumini katika mfungo.
Wafanyabiashara wanaopandisha bei za vyakula vinavyotumiwa na waumini, wanasababisha mzigo mzito kwa familia nyingi.
Katika kipindi hiki cha Ramadhani, ni muhimu kwa wafanyabiashara kujiepusha na vitendo vya kupandisha bei.
Badala yake, wanapaswa kuwa na moyo wa huruma na ushirikiano kwa kuzingatia kwamba waumini wanahitaji chakula na mahitaji mengine kwa bei nafuu ili waweze kufunga kwa amani.
Kwa hivyo, tunawahamasisha wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kuwa na uvumilivu na kusaidia kuleta utulivu katika kipindi hiki.
Hii itachangia katika kujenga umoja na mshikamano katika jamii na muhimu zaidi, itaongeza amani na upendo miongoni mwa Watanzania.
Tunawasihi watu binafsi au kikundi chochote kinachojishughulisha na biashara, kisitumie kipindi hiki cha mfungo kama fursa ya kutengeneza faida nono kupitia bidhaa zinazotumika zaidi.
Kama ilivyo ada ya Watanzania, ushirikiano na umoja udumu na kuhakikisha mfungo wa Ramadhani unatekelezeka bila kukamua mifuko ya waumini kutokana na ongezeko la bei. Tunawatakia Waislamu wote mfungo mwema.
Hi there,
We run a Youtube growth service, where we can increase your subscriber count safely and practically.
– Guaranteed: We guarantee to gain you 700-1500 new subscribers each month.
– Real, human subscribers who subscribe because they are interested in your channel/videos.
– Safe: All actions are done, without using any automated tasks / bots.
– Channel Creation: If you haven’t started your YouTube journey yet, we can create a professional channel for you as part of your initial order.
Our price is just $60 (USD) per month and we can start immediately.
If you are interested then we can discuss further.
Kind Regards,
Katelyn
Hi,
I just visited habarileo.co.tz and wondered if you’d ever thought about having an engaging video to explain what you do?
Our prices start from just $195.
Let me know if you’re interested in seeing samples of our previous work.
Regards,
Joanna
Unsubscribe: https://removeme.live/unsubscribe.php?d=habarileo.co.tz