Tanzania kuendeleza mapinduzi ya elimu

VIENNA, AUSTRIA : TANZANIA imeahidi kuendeleza mapinduzi ya kidigitali katika sekta ya elimu kupitia ushirikiano na Kampuni ya eee Austria.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, amesema serikali iko tayari kutumia teknolojia za TEHAMA katika ngazi zote za elimu ili kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza. SOMA: Mfumo wa zabuni kidigitali kuleta ushindani kwa wajasiriamali
Prof. Nombo alitoa kauli hiyo alipokutana na Afisa Mkuu Muidhinishaji wa Miradi wa Kampuni ya eee Austria, Bi. Theresa Wutz, ambapo alishukuru hatua ya Austria kupitia UniCredit–Bank of Austria kuendelea kufadhili Mradi wa Elimu Kidigitali Zanzibar.
Alisema msaada huo utafungua fursa za kupanua matumizi ya TEHAMA hadi shule na vyuo vya Tanzania Bara, na kuongeza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha walimu na wanafunzi wananufaika na teknolojia hizo.