Mashabiki wa soka kupata zawadi kampeni amsha amsha

DAR ES SALAAM. Mashabiki wa soka wa Tanzania, sasa wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha kupitia kampeni ya  Amsha Amsha iliyozinduliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania kampuni ya simu ya Halotel.

Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul amesema kuwa mbali ya zawadi ya fedha ya Sh 50,000 kwa washindi wawili kwa siku, pia mashabiki wa soka wanaweza kujishindia fedha taslimu, simu janja, na televisheni za kisasa.

Paul amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wao ambapo pia wanaweza kushindia fedha kwa kubashiri matokeo ya mechi katika ligi mbalimbali duniani.

Advertisement

“Washindi wawili wa kila siku watajishindia Sh 50,000, ambapo jumla ya Sh 6,000,000 zimetengwa kwa kipindi hiki cha sikukuu,” amesema Paul.

Ameongeza kuwa kila mwisho wa wiki kutakuwa na droo maalum ambapo washindi wawili watajishindia simu janja ya Samsung A-Series yenye thamani ya Sh 500,000.

Zaidi ya hayo, wateja pia watapata nafasi ya kujishindia televisheni za kisasa aina ya Hisense zenye thamani ya Sh1.2 milioni kila moja, ambapo jumla ya televisheni nane zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu ya promosheni.

Alisema kuwa shabiki wa soka anaweza kuingia kwenye droo kwa kujisajili kupitia tovuti yao, www.m-bet.co.tz, kuweka pesa kupitia HaloPesa, na kubeti kwa dau la kuanzia Sh 2,000 ili kuingia kwenye droo.

Ofisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, amesema, “Tunafurahi kushirikiana na M-Bet kwenye promosheni hii. Lengo letu ni kutoa fursa kwa wateja kufurahia michezo ya kubashiri kupitia HaloPesa, ambayo ni njia rahisi na salama ya kufanya malipo. Promosheni hii itaunganisha burudani ya kubashiri na urahisi wa huduma za malipo ya simu.”

Lwiza aliongeza kuwa promosheni hii itawawezesha wateja wa HaloPesa kufurahia huduma za M-Bet na kuingia kwenye droo za zawadi za kila siku, wiki, na mwezi.

Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania, Levis Paul (kulia) akizungumzia kampeni ya Amsha Amsha ambayo  wanashirikiana na kampuni ya simu ya teja na Halotel kupitia HaloPesa. Kushoto ni Ofisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza.