Mauaji mapya ya ADF yatikisa DRC

DR CONGO: UMOJA wa Mataifa umesema takriban raia 52 wameuawa na waasi wa ADF katika mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa taarifa ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), mashambulizi hayo yalifanyika kati ya Agosti 9 na 16 katika vijiji kadhaa vilivyoko Jimbo la Kivu Kaskazini.

MONUSCO imeonya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka, ikikumbusha kuwa mwishoni mwa Julai waasi hao waliwaua zaidi ya watu 40 ndani ya kanisa mjini Komanda, karibu na Jimbo la Ituri. SOMA: Waasi wa ADF wauwa zaidi ya watu 40

Mbali na mauaji, ADF iliripotiwa kuwateka nyara raia, kupora mali na kuchoma nyumba, magari pamoja na pikipiki. Mashambulizi haya yametokea huku DRC pia ikikabiliwa na mzozo mwingine na waasi wa M23 katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button