Mashine mpya kurahisisha uchakataji taarifa MUHAS

DAR ES SALAAM: Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimepokea kompyuta kuu tatu za ‘Lambda Vector’ zitakazotumika kutafuta, kuchakata taarifa na kurahishisha njia za kugundua magonjwa na matibabu kwa kutumia akili unde.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 30, 2025, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema vifaa hivyo yenye thamani ya Sh milioni 40, vimetolewa na Shirika la Global Health Labs (GHL) la Washington Marekani, kwa ushirikiano kati ya Bill & Melinda Gates Foundation na Gates Ventures.
Prof Kamuhabwa amesema kompyuta hizo pia zitatumika kuboresha mazingira ya kufundishia, lakini pia kuboresha maisha wa Watanzania.
“Tunakuwa na taarifa za wagonjwa wengi sana, sasa taarifa zile zinaingizwa kwenye computer, zinachakatwa, zinakuja kutoa mpango kwamba kwa ugonjwa huu ukitaka kuutambua utatumia vigezo hivi, au matibabu yake ni haya,” amesema Prof Kamuhabwa.
“Badala ya daktari kukaa na kusoma vipimo mwenyewe, ikishathibitisha mashine inaweza kutumia taarifa mlizoziweka inamrahisishia daktari, ugonjwa huu ninavyouona kutokana na taarifa kwa asilimia 95-98 ni ugonjwa fulani lakini unaweza kutibika kwa njia fulani.
Prof Kamuhabwa amesema mchakato huo utawarahisishia Watanzania waishio maeneo ya vijijini ambao watatakiwa kusafiri kwa magonjwa mbalimbali kwenda hospitali kubwa, kwani wataweza kusoa taarifa zao kwa wakati.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa Tiba MUHAS, Deogratias Mzurikwao, ameeleza kuwa amesema kompyuta hizo zina uwezo mkubwa na zinafanya kazi kwa muda mfupi tofauti na ambazo walikuwa wakizitumia.
“Tunazo tisa tayari, lakini zina uwezo mdogo kulinganisha na hizi tatu tulizozipata, ambazo kutokana na kazi zile za mwanzo, ndizo zimeweka kutusaidia kupata hizi tatu mpya,” amesema Mzurikwao.
Amesema tayari wana teknolojia ya utambuzi wa kansa ya titi, hivyo ujio wa kompyuta hizo utasaidia ugunduzi wake, lakini itasaidia katika kutekeleza ugunduzi wa teknolojia ya magonjwa ya moyo ambayo ipo kwenye majaribio.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com