Samia, Nchimbi walivyorejesha fomu INEC

UREJESHAJI wa fomu na uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais umefanyika leo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo eneo la Njedengwa, Dodoma.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dk Emmanuel Nchimbi walikuwa wa mwanzo kurejesha fomu hizo na kisha kuteuliwa rasmi na INEC kuwa wagombea kupitia CCM.

Mchakato huo unafanyika kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 50 na 62 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, vikisomwa pamoja na kanuni ya 23 na 26 za Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025.



