‘Matumizi ya gesi kupikia ni lazima isiwe anasa’

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema matumizi ya gesi ya kupikia ni lazima kwa sasa na sio anasa kama ilivyokuwa zamani, lengo ni kuondoa madhara ya kiafya na kimazingira yanayochochewa na matumizi ya nishati chafu ya kupikia kama vile mkaa na kuni.

Rais Samia amesema hayo leo Mei 08, 2024 kwenye uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia wa Mwaka 2024-2034 uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Wengi hawatumii nishati safi kwa sababu ya gharama na uhakika wa upatikanaji. Niwaase sekta binafsi kusogeza huduma zaidi, ili iwe rahisi kwa wananchi wa vijijini kupata gesi kwa wepesi,” amesema Rais Samia.

buy lasix online http://gmaxind.com/assets/jpg/lasix.html no prescription pharmacy

Amesema sababu hizo zinaweza kutatuliwa kwa njia ya ushirikiano miongoni mwa mamlaka mbalimbali za kiserikali na binafsi ikiwemo kutumia teknolojia itakayosaidia upatikanaji rahisi wa gesi kwa bei nafuu.

“Safari yetu ya kimaendeleo haiwezi kupiga hatua ikiwa asilimia 90 ya wenzetu bado wanatumia nishati isiyo rafiki kwa mazingira, nishati na uchumi,” ameasa Rais Samia na kuwataka wananchi kubadili fikra ya matumizi ya gesi, kwani wanaweza kupika vitu vingi kwa kutumia gesi.

buy xtandi online http://gmaxind.com/assets/jpg/xtandi.html no prescription pharmacy

“Kuna imani kuwa ladha ya chakula cha kupikia gesi na mkaa, kuni ni tofauti, hiyo ni Imani tu,” amesema.

buy rifadin online http://gmaxind.com/assets/jpg/rifadin.html no prescription pharmacy

Hata hivyo, amewataka Mama Lishe kujikita zaidi katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, huku akiwaasa wawe na lugha nzuri yenye ushawishi kwa wateja wao wanaotaka matandu katika wali.

Rais Samia amewaasa wananchi kudumisha upandaji miti nchini ili kufidia uharibifu uliokwishafanyika kutokana na shughuli za kila siku, ikiwemo ukataji miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.

Habari Zifananazo

Back to top button