Mavunde atoa maelekezo 5 kwa Stamico

ataka utekelezaji si maneno

DODOMA: WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ametoa maagizo matano kwa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) ili kuendana na kasi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mavunde ametoa maagizo hayo  akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO jijini Dodoma ambapo aliiagiza STAMICO  kuwaendeleza na kuwasimamia wachimbaji wadogo

Pili ameitaka STAMICO kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo na kuhakikisha wanapata mitambo na vifaa maalum vya uchimbaji.

“Hakikisheni mnawasimamia kikamilifu wachimbaji wadogo na hasa katika kutatua matatizo yao ya msingi ili waweze kukua katika shughuli zao za uchimbaji,”amesema Mavunde.

Mavunde ameagiza pia mitambo na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuwahudumia wachimbaji wadogo viwekewe utaratibu mzuri na wa wazi ili viendelee kuhudumia kundi kubwa zaidi la wachimbaji.

“Hakikisheni mnaendelea kuwasaidia vifaa wachimbaji hawa ili waongeze tija ya uzalishaji,”amesisitiza

Aidha, Mavunde amewataka STAMICO kuharakisha mchakato wa uanzishishwaji wa benki ya wachimbaji ili kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa achimbaji.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo akitoa taarifa amesema,  STAMICO imeongeza mapato makubwa ndani ya muda mfupi kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Shirika linaendelea kulifanya na hivyo kulitoa kuwa sehemu ya mashirika tegemezi na kuwa Shirika litasimamia maagizo na maelekezo ya Wizara katika kujiimarisha na pia kuendeleza ulezi wenye tija kwa wachimbaji wadogo.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button