MC.Pilipili: Kifo cha mama kilinitoa kazini

MCHEKESHAJI maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu MC Pilipili amesema vifo vya mama yake mzazi na mama yake mdogo vya ajali ya gari wakati wa harusi ya mdogo wake vilimlazimisha kupumzika kufanyakazi zake za uchekeshaji kwa takribami miaka mitatu kutokana na majonzi aliyokuwa nayo.

Mc Pilipili amesema mwishoni mwa mwaka jana ndiyo alianza upya kurudi rasmi katika kazi yake ya uchekeshaji huku akijinadi kwamba huenda mwaka huu wa 2024 ukawa wa mafanikio makubwa kwa tasnia nzima ya uchekeshaji.

“Kifo cha mama kiliniumiza nikalazimika kuwa kimya kwa muda mrefu takribani miaka mitatu lakini sasa nimerudi na mwaka 2024 nauona kuwa mwaka wa mafanikio kwa tasnia yetu ya sanaa ikiwemo uchekeshaji,” amesema MC Pilipili.

Amesema sanaa ya uchekeshaji kwa mwaka huu itafanya vizuri zaidi kwa kuwa imefanya vizuri sana kwa mwaka jana ambapo wachekeshaji wapya wenye uwezo mkubwa wameibuliwa hivyo mwaka huu ni mafanikio tu kwa wachekeshaji.

 

Habari Zifananazo

Back to top button