Mfumo waongeza ufanisi, mapato wadau wa sanaa

DAR ES SALAAM: WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imefanikisha uunganishaji wa mfumo wa wadau wa sanaa (AMIS) na mfumo wa TAUS, hatua ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma kwa wadau wa sanaa pamoja na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Akizungumza katika kikao kazi cha 15 cha Maofisa Utamaduni na Maofisa Maendeleo ya Michezo wa Tanzania Bara, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amesema kuwa kupitia mifumo hiyo, wadau katika maeneo 15 ya biashara ikiwemo studio za muziki, picha, video, huduma za burudani na ubunifu sasa wanaweza kupata vibali kwa njia ya moja kwa moja na kwa haraka zaidi.

Mwinjuma ameeleza kuwa, matokeo chanya ya matumizi ya mifumo hiyo tayari yameanza kuonekana, ambapo mapato ya Baraza la Sanaa la Taifa yameongezeka kwa asilimia 200.

Amebainisha kuwa Sheria ya Fedha Na. 6 ya mwaka 2022 inaruhusu kuanzishwa kwa kampuni binafsi zitakazokuwa na jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha kwa pamoja, jambo linalolenga kuongeza uwazi na haki kwa wabunifu wa kazi za sanaa.

Sheria hiyo pia imeanzisha chanzo kipya cha mapato kinachojulikana kama tozo ya hati miliki, ambacho hukusanywa kutokana na uingizaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha, kubeba na kusambaza kazi za wabunifu.

Kupitia chanzo hicho, kwa mwaka wa fedha 2023/2024, COSOTA ilikusanya zaidi ya shilingi milioni 847. Kwa mwaka huu wa fedha, kiasi kilichokusanywa ni zaidi ya shilingi milioni 628, na hivyo kufikisha jumla ya shilingi bilioni 1.4.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I’m getting 88 D0llars consistently to deal with net. Q I’ve never accepted like it tends to be reachable anyway one of my most noteworthy buddy got D0llars 27,000 D0llars in three weeks working this basic task and she impacted me to avail…
    Take A Look Here….> http://Www.HighProfit1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button