Mgombea aahidi kutatua changamoto, maji barabara

MKINGA, Tanga: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkinga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Twaha Mwakioja amewahidi wananchi wa eneo hilo kuwa endapo watamchagua atakwenda kutatuta changamoto ya maji na barabara, ambayo ndio kero kubwa kwa wakazi wa hao kwa muda mrefu.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni zake uliofanyika jana katika uwanja wa Mapatano wilayani Mkinga mkoani Tanga, Mwakioja alisema suala jingine ni changamoto ya ajira,hivyo kwa kutumia fursa ya bahari na misitu ya ataweza kuanzisha miradi itakayowanyanyua wananchi kiuchumi.
Kwa upande wa changamoto ya barabara alisema anafahamu kuhusu uwepo wa changamoto ya barabara ya kutoka Mkinga kwenda Tanga,hali yake sio nzuri hivyo akipewa ridhaa na wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge atakwenda kutatua kero hiyo,kwani tayari ipo mipango na kilichobakia na usimamizi.
SOMA ZAIDI
Akifungua kampeni hizo Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Omar Ayoub alisema ipo miradi mingi ya maendeleo kwenye mkoa huo ambayo inagusa ustawi wa wananchi ndio maana chama hicho kimesimamisha wagombea kote wakayasimamie.
“Chama kinatambua changamoto ya Jimbo la Mkinga ndio maana kimechagua Mwakioja kuwa mwakilishi kwani anauwezo mkubwa na ushawishi wa kuweza kuwasemea wanamkinga ikiwemo kusimamia maendeleo yenu,”alisema mjumbe huyo.



