Mgombea CCM ameahidi ukamilishaji wa miradi

MWANZA: MGOMBEA wa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Misungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Silvery Luboja ameahidi kushirikiana kwa karibu zaidi na Serikali pamoja na wakazi wa Wilaya ya Misungwi kwa kuhakikisha wanakamilisha miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Luboja amesema hayo leo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mamaye kata ya Mamaye wilayani Misungwi. Mgombea huyo amesema katika Wilaya ya Misungwi kuna miradi 30 ya maendeleo inaendelea na bado haijakamilika.
Ameahidi atashirikiana na Serikali ili kuweza kukamilisha miradi hiyo itakayoweza kuleta maendeleo kwa wakazi wa Misungwi.
‘’Nahidi wakazi wa kata ya Mamaye nitafuatlia kwa ukaribu zaidi ili tuweze kupata umeme katika kata yetu. Pia tutakamilisha ujenzi wa Zahanati ya Mwalige’’ amesema.

Luboje ameahidi kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ili waweze kurekebisha Barabara ya kutoka Misungwi kupitia Mwambola kuelekea Kolomije.
Upande wa tatizo la maji, Luboja amesema watakamilisha ujenzi mkubwa wa mradi wa maji kutokea Ukiliguru kupitia Kolomije na kuelekea mpaka maeneo ya kata ya Bulemeji.
Naye Mgombea udiwani wa kata ya Mamaye kupitia CCM,Yohana Shimbeyangoso amesema atashirikiana na mgombea Ubunge wa CCM, Silvery Luboje ili waweze kutatua kero za wakazi wa kata ya Mamaye.



