Mgombea ubunge aahidi maendeleo Ngorongoro

ARUSHA: MGOMBEA ubunge Jimbo la Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi{CCM) aliyepita bila kupingwa katika jimbo hilo, Yannick Ndoinyo amesema kuwa mara baada ya kuapishwa bungeni atashirikiana na serikali na wananchi na kuhakikisha anafanya mabadiliko makubwa ya maendeleo katika jimbo hilo

Ndoinyo alisema hayo akiwa katika kata za Olorieni, Maaloni na Malambo katika ziara yake na viongozi wa CCM wilaya katika harakati za kumwombea kura mgombea urais wa chama hicho Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa wananchi wa jimbo hilo wana changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa kwa kushirikiana na serikali.

Alisema Ilani ya CCM imetenga miradi mikubwa ya maendeleo, katika Jimbo hilo na baadhi yao bado haijakamilika pamoja na kwamba fedha zimeshatolewa na akasisitiza kuwa atahakikisha miradi yote iliyosalia inakamilishwa ili wananchi waweze kufurahia matunda ya serikali yao itakayowekwa madarakani mara baada ya octoba 29 mwaka huu.

Ndoinyo ameahidi kuwajengea mazingira mazuri wafugaji wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na wananchi kuwezeshwa kwa kupata mikopo nafuu na mitaji ya biashara, pamoja na kujenga kiwanda cha kusindika nyama, kitakachowawezesha wafugaji kupata thamani zaidi ya mifugo yao.

Alisema na kuwataka wananchi kumchagua mgombea urais wa CCM kwani ana mipango mizuri ya maendeleo katika Jimbo la Ngongoro na nchi kwa ujumla na kuwakataa wagombea wa upinzania ambao hanawa sera wala dira.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Lucas Olemasiaya, amewataka wananchi wa jimbo hilo na vitongoji vyake kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya octoba 29 mwaka huu katika vituo vya kupiga kura ili wamchague mgombea urais wa CCM sambamba na mbunge na diwani ili waweze kutekeleza malengo waliyoyapanga kwa maslahi ya wananchi.

Olemasiaya alisema hakuna chama chenye mipango madhubuti katika nchi hii kama CCM na kusema kuwa vyama vingine vinafanya siasa za propaganga na kuwataka wananchi kuhakikisha kata mbili za Jimbo hilo za sale na Oldonyosambu wapinzania wamechukua fomu kuwani udiwani wanapigwa chini ili wajue chama tawala iko kila mahali

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button