Mgombea ubunge asifu serikali ujenzi barabara DODOMA Mjini

DODOMA : MGOMBEA Ubunge jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pascal Chinyele ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kusimamia ujenzi wa barabara zote jimboni humo kwa kiwango cha lami. Chinyele alitoa shukurani hizo kwenye mkutano wa kampeni ya mgombea wa urais kupitia chama hicho, Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma .

Alishukuru kwa uamuzi wa kusimamia ujenzi wa barabara ya mzunguko ambayo eneo la pembezoni litatumika kujenga viwanda. Chinyele alimpongeza Rais Samia kwa kujenga hospitali ya kisasa ya wilaya ya Dodoma mjini iliyogharimu Sh bilioni mbili na kukamilisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kituo kikuu cha mabasi reli hiyo ambacho kimekuwa kivutio cha uchumi wa vijana mkoani humo.

Alimpongeza kwa kutanua Soko la Majengo, kusimamia ujenzi wa soko la Wamachinga na kugawanya Jimbo la Dodoma kwa kutoa majimbo mawili ya Dodoma Mjini na Mtumba. Alisema uamuzi huo utasaidia kupunguza changamoto za wananchi wa majimbo hayo. Chinyele alimuomba mgombea huyo wa urais kama atashinda katika uchaguzi kama atashinda katika uchaguzi huo, asaidie ijengwe barabara inayotoka Namba One kuelekea Tarafa ya Zuzu hadi Singida katika kipande cha kilometa nane kutoka Namba One hadi Bihawana.

Aliomba pia ujenzi wa vituo vya afya kwenye kata ya Zuzu, Matumbulu, Mpunguzi, Mbabala na Chididimo. Awali, aliyekuwa mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde ambaye kwa sasa anagombea Jimbo la Mtumba kupitia CCM, alimshukuru Samia kwa kuwajengea shule mpya tisa za sekondari na saba za msingi. Pia, alipongeza ujenzi wa madarasa 800 yenye thamani ya Sh bilioni 18 pamoja na ujenzi wa shule za ghorofa.

Alisema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia kwenye sekta ya afya amejenga vituo vya afya katika kata kadhaa pamoja kuboresha Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuanzisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo matibabu ya saratani. SOMA: Dodoma tayari kwa mabalozi, serikali yatoa viwanja bure

“Kwenye sekta ya maji tulikuomba uchimbaji wa visima virefu vya maji na tayari vimechimbwa lakini pia kwenye sekta ya nishati umehakikisha mitaa yote ya Dodoma ina umeme na kuna mradi wa kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo yote ya mkoa huo,” alisema Mavunde. Kwenye sekta ya michezo, Mavunde alisema Rais Samia amejenga uwanja mkubwa wa kimataifa uliopo Nzuguni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kilimani hadi Chamwino. Mavunde alisema serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuongeza mtandao mrefu wa barabara za lami. Pia Sh bilioni 600 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba.ambazo zimechangamsha uchumi.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Burkina Faso bans homosexuality as a crime punishable with prison, fines

    In the new law, those found guilty of homosexuality could face a two- to five- year prison sentence.

    Burkina Faso President Ibrahim Traore.
    Burkina Faso President Ibrahim Traore arrives to the Grand Kremlin Palace in Moscow, Russia, on May 10, 2025 [Stanislav Krasilnikov/RIA Novosti via AP]

    Published On 2 Sep 2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button