Mgombea ubunge CCM aahidi karakana la ujuzi mjini Geita

GEITA: MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Chacha Wambura ameahidi iwapo atachaguliwa atafanikisha ujenzi wa karakana kwa ajili ya vijana kupata ujuzi na maarifa.
Mhandisi Chacha ametoa ahadi hiyo katika mkutano wake wa kufunga kampeni za uchaguzi uliofanyika viwanja vya soko la Nyankumbu mjini Geita na kueleza Karakana hiyo itasaidia matumizi sahihi ya mikopo ya halmashauri.
Amesema serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa kufanikisha utoaji wa mikopo ya makundi maalum ikiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu lakini ili izae matunda ni vyema vijana wapate ujuzi na maarifa.
Amesema karakana hiyo itawajengea uwezo vijana kuweza kutekeleza miradi kulingana na ujuzi wao na kupunguza tatizo la ukopeshaji usio na tija ambao unapelekea vijana wengi kushindwa kurejesha mikopo wanayopatiwa.
Ameongeza, pia amejipanga kikamirifu kusimamia mpango wa utoaji wa mikopo ya makundi maalum kutoka asilimia 10 ya mapatoa ya halmashauri utekelezwe kwa usawa na na haki kwa wenye uhitaji hasa kina mama na walemavu.
Amesema kupitia taaluma yake ya uhandisi ataisaidia serikali kusimamia wakandarasi wote wenye tenda za ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara waweze kuwajibika kwa mjibu wa matakwa ya mkataba.
Ameahidi kuwa atasimamia maendeleo na ujenzi wa huduma za kijamii hususani elimu, afya na maji ziendane na hadhi ya mji wa Geita ambao umepandishwa na kuwa manispaa kwani mapato ya ndani na nje yameongezeka.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande amesema chama kina imani na wagombea wote kuanzia nafasi ya urais, ubunge na udiwani hivo wananchi hapaswi kuwa na mashaka badala yake wajidae kupiga kura.
Mapande amesisitiza kuwa serikali ya CCM imejizatiti kuboresha huduma za kijamii mjini Geita na ndio maana serikali ya awamu ya sita imetoa pesa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara, maji na elimu.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com