Mgombea ubunge Hanang aomba kiwanda cha nafaka

MANYARA: Mgombea ubunge Jimbo la Hanang kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asia Halamga, ameomba ujenzi wa kiwanda cha nafaka ili kukuza uchumi kwa wananchi.
Asia amewasilisha maombi hayo kwa Mgombea Urais Dk Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni za kunadi sera za chama hicho.
”Tunayo raslimali ya kutosha,tunayo malighafi ya kuzalisha saruji yenye zaidi ya miaka mia moja ambayo ikifanyiwa process tuna uchumi wa viwanda wa kutosha. Tatizo letu ni ukosefu wa viwanda vya kuchakaa malighafi hizo,tunakosa kiwanda,”amesisitiza Halamga.
Hanang ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Manyara ambazo zinazalisha mazao mengi ya biasharaikiwemo ngano, dengu, maharage na alizeti.



