Mgombea ubunge Monduli amkumbuka Lowasa

ARUSHA: MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha, Joseph Isack maarufu kwa jina la ‘Kadogoo’ amesema kuwa anamshukuru Hayati Edward Lowassa katika harakati za siasa kwani aliwahi kumtabiria kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kadogoo ametoa siri hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya kugombea jimbo hilo iliyofanyika eneo la Esilaley Kata ya Elsilaley katika Mji wa Kigongoni wilayani Monduli mapema leo.

Amesema yeye ni zao la Hayati Lowassa na hayo matunda aliyoyapata katika siasa ni mchango wake mkubwa na hakusita kunitabiria kuwa iko siku atakuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli.

‘’Lakini naomba niseme neno na ninaweza nisieleweke lakini nisiposema naweza nisiitendee nafasi yangu na nalisema hili kutoka ndani ya sakafu ya moyo wangu,” amesema.

’’Sisi wana Monduli hasa sisi wanasiasa nisipomtaja Hayati Edward Lowassa sitakuwa nimeitendea haki nafsi yangu kwanini sisi ni zao lake kwani sisi ni matunda yake na huko aliko akasikia ama akiamka na kunikuta mie ni moja ya mazao yake kewa kweli atafuraji na kufarijika sana,” amesema Kadogoo.

Kadogoo amesema kuwa Hayati Lowassa atakumbukwa na wanasiasa wengi katika Jimbo la Monduli wakiwemo madiwani waliteuliwa katika kinyang’anyiro hicho na wengine walioshika nyadhifa mbalimbali kiwilaya, mkoa na taifa aliowawahi kuwatengeneza yeye.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button