Mgombea urais CUF: Pigeni kura, msisuse

TANGA: Mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Semandito Gombo amewataka watanzania kutosusia uchaguzi mkuu kwani mabadiliko ya kweli yanatokana katika sanduku la kura.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu tathimini ya awamu ya kwanza ya kampeni za ugombea urais,ubunge na udiwani

Amesema ni muhimu wapuuzie watu ambao wanafanya ushawishi wa kususia uchaguzi na kufanya maandamano ambayo yatasababisha kuvuruga amani iliyopo.

“Niwaombe watanzania jitokezeni kushiriki kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu kama kweli mnataka kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya amàni na utulivu “amesema Mgombea huyo urais.

Aidha, amesema kuwa katika siku 100 atakapoingia Ikulu uongozi atahakikisha anaunda tume ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya ili kumaliza changamoto huyo ambayo ni kilio cha watanzania kwa muda mrefu.

“Ndani ya siku 100 za uongozi wangu nitahakikisha nasimamia elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu sambamba na kudhibiti mianya ya rushwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button