Miaka 10 ya TBPL, kilimo, afya mambo safi

PWANI: SERIKALI imesema Kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd (TBPL) kimekuwa nguzo muhimu katika sekta ya afya na kilimo kwa kuzalisha viuatilifu vya kibaiolojia vinavyotumika kupambana na mb’u waenezao malaria na wadudu waharibifu wa mazao.
Akizungumza leo Oktoba 16, 2025 wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 10 ya kiwanda hicho mkoani Pwani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah, amesema TBPL ni mfano bora wa utekelezaji wa sera za viwanda na ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi.
“Kupitia uzalishaji wa TBPL tumeshuhudia uzalishaji wa maelfu ya lita za viuatilifu vya kibaiolojia kwa mwaka, kuongezeka kwa uwezo wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko, kuongeza ajira lakini pia TBPL imekuwa na mchango mkubwa katika utafiti, ubunifu na ujenzi wa uwezo wa wataalamu wazawa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Abdallah.
Aidha, Abdallah, ameongeza kuwa kwa miaka 10 TPBL imekuwa mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwamba ni mfano halisi wa jinsi sera za viwanda za serikali zinazoweza kuleta matokeo chanya kama zitatekelezwa kwa nidhamu, uwajibikaji na ubunifu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TBPL, Dk. Allan Ulula amesema kiwanda hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa mtu mmoja na kwa Taifa kwa ujumla, kwa kusaidia kutunza afya kwa kuzuia malaria pamoja na kutoa mchango kwenye uzalishaji kupitia bidhaa kama mbolea.
Pia Dk. Allan ameishukuru serikali kwa jitihada za kukianzisha kiwanda hicho, kukisimamia, kukikuza na kukitunza kwa miaka 10, pamoja na kuwa kinara wa manunuzi ya bidhaa za kiwanda hicho.
Meneja Mkuu wa TBPL, Injinia Rafael Rodriguez, amesema katika miaka 10 ijayo, kiwanda kimepanga kuongeza uzalishaji na kuimarisha usambazaji wa dawa, huku akiomba Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kusaini mikataba ili kurahisisha upatikanaji wa dawa hizo.
Rodriguez amebainisha kuwa kiwanda hicho ni alama ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba, na serikali ya Cuba imeahidi kuendelea kuleta teknolojia mpya kiwandani hapo.
SOMA ZAIDI: Serikali sasa yamiliki kiwanda cha TBPL asilimia 100
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dk. Nicholas Shombe, amesema TBPL ina uwezo wa kusambaza viuatilifu katika zaidi ya nchi saba ikiwemo Kenya, Msumbiji, Botswana, Nigeria, Niger, Angola, Bangladesh na Sri Lanka.
“Tumeongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za Kibaiolojia zinazotumika katika sekta ya afya na kilimo. Tumeajiri na kuwajengea uwezo vijana zaidi ya 200 wa Kitanzania katika nyanja za sayansi, utafiti, na teknolojia.Tumewekeza katika miundombinu ya kisasa ya maabara na viwanda, vinavyokidhi viwango vya kimataifa. Tumechangia katika kuimarisha afya ya jamii kupitia bidhaa salama, zenye ubora, na zinazozalishwa hapa nchini” amesema Dk. Shombe.
Mfamasia Mkuu wa Serikali, David Masasi, amesema TBPL tayari imepokea Shilingi bilioni 11.5, na kwenye bajeti ya mwaka huu imetengewa bilioni 10 zaidi. Amesema tangu kuanza kwa matumizi ya dawa hizo, kiwango cha maambukizi ya malaria kimepungua kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi asilimia 8.1 mwaka huu.
Masasi ametoa wito kwa uongozi wa kiwanda kuhakikisha wanaendelea kuimarisha uzalishaji na ubora wa bidhaa ili kufikia masoko ya kimataifa. Pia amewataka wananchi kutumia dawa hizo kwa usahihi kwa lengo la kutokomeza malaria nchini.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com