Migiro, Kikwete waeleza sababu CCM kuchaguliwa

PWANI : KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk AshaRose Migiro ameweka wazi sababu za chama hicho kuchaguliwa kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Dk Migiro alitoa kauli hiyo jana wakati wa kampeni za kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wengine wa chama hicho, zilizofanyika mkoani Pwani. “Sababu za wazi zimeelezwa na wabunge, lakini kubwa zaidi ni kwamba katika uongozi wake maendeleo yamepatikana, miundombinu imejengwa na ustawi wa wananchi umeonekana. Mnafahamu wazi namna Mkoa wa Pwani ulivyokuwa lango la taifa kwa karne nyingi,” alisema Dk Migiro.
Aliongeza kuwa mji wa Bagamoyo umekuwa kitovu cha biashara na historia ya ukombozi wa Afrika, huku Mkoa wa Pwani kwa ujumla ukiendelea kuwa kitovu cha utalii kupitia Kisiwa cha Mafia, fukwe za Bagamoyo, hifadhi za Rufiji na urithi wa asili wa utamaduni unaoitangaza Tanzania kimataifa.
Dk Migiro alisema vivutio hivyo vimekuwa sehemu ya simulizi ya filamu ya ‘Tanzania: The Royal Tour’, iliyoandaliwa na kusimamiwa na Samia hivyo kuchangia katika kukuza pato la taifa kupitia sekta ya utalii. “Vitu vyote hivyo vinaendelea kuipa sifa Tanzania na kuitangaza kimataifa. Ni wazi kuwa mambo makubwa yamefanyika na yanaonekana,” alisema. SOMA: ‘Kufikisha ujumbe kwa maandamano hakuleti chakula’
Alisema mgombea wa chama hicho amefanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 na kuendeleza huduma za jamii kwa kuzingatia utu. Naye Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema kutokana na mafanikio ya utekelezaji wa Ilani aliyofanya Samia, Pwani itampa kura za kutosha na Watanzania wasisite kumchagua. Alisema Samia ametekeleza Ilani kwa kuzingatia utu katika nyanja zote.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com