Mikataba wafanyakazi wa nyumbani kilio cha wengi

DAR ES SALAAM; MIKATABA ya maandishi ya ajira kwa wafanyakazi wa nyumbani imetajwa kuwa ni kilio cha wengi kisichokuwa na matumaini kutokana na waajiri wengi kukwepa kuingia makubaliano nao licha ya sheria kutaka hivyo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya mwaka 2004, inaeleza mfanyakazi yeyote anayefanya kazi kwa zaidi ya saa 45 kwa wiki anapaswa kuwa na mkataba wa ajira na alipwe posho ya saa za ziada

Suala hilo limeibuliwa baada ya viongozi wa elimu rika wa wafanyakazi wa nyumbani wapatao 25 kutoka mikoa sita kuwasilisha malalamiko hayo katika warsha ya mafunzo ya wafanyakazi hao yaliyoratibiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) kwa kushirikiana na Serikali na Chama cha Wafanyakazi wa Majumbani, Hifadhi, Hotelini, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU).

Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Nyumbani Mkoani wa Morogoro, Desdelia Simon amesema ukosefu wa mkataba wa maandishi ni moja ya changamoto kubwa ambayo wanakumbana nayo, huku mkataba huo ukibeba haki zao.

Jenifer Mtanga mfanyakazi wa nyumbani kutoka mkoani Dodoma amesema kwa upande wake ndani ya mwaka mmoja amepata mwajiri ambaye tayari ameingia nae mkataba wa maandishi katika kufanya kazi nae.

Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya Sheria kutoka CHODAWU Taifa, Asteria Gerald amesema mkataba ni nguzo kubwa ya majadiliano baina ya mwajiri na mfanyakazi wa nyumbani katika kulinda haki ya kila mmoja.

Naye Muamuzi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Herman Komba amesema sheria ya kazi,ajira na uhusiano mahali pa kazi imeeleza namna ambavyo mahusiano ya kiajira inavyotakiwa kuanza kwa muajiri kutoa mkataba wa ajira kwa mfanyakazi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    More Details For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button