RAIS Samia Hassan Suluhu ametoa Sh milioni 10 kwa uongozi wa waendesha bodaboda Wilaya ya Arusha kwa ajili ya kuanzisha chama cha ushirika ikiwemo pikipiki mbili zitakazosaidia utatuzi wa changamoto zao.
Pia waendesha bodaboda waiomba serikali kupunguza gharama za awali za ukataji wa leseni ya udereva hadi kukamilika kwake kutoka Sh 99000 na kufikia Sh 30000 ili kila mmoja aweze kumiliki leseni.
Fedha hizo zimetolewa leo Jijini Arusha na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Mohamed Ali Kawaida wakati wa Mkutano Maalum kwa ajili ya elimu ya ushirika wa bodaboda ikiwemo kuzindua mfumo wa kidigitali wa utambuzi wa maofisa hao.
Kawaida amesema Rais pia licha ya kutoa fedha hizo pia ametoa pikipiki mbili kwa uongozi wa maofisa usafirishaji ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa aajili ya kusikiliza changamoto za maofisa hao kwenye kata mbalimbali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha, Mrisho ametoa Sh milioni 10 kwaaajili ya kuchagia mfuko wa chama cha bodaboda wilaya ya Arusha na kusisitiza kuwa miaka minne bado wahusika waliokula fedha za umoja huo hawajakamatwa wahusika huku wakijulikana.
Amemuomba Kawaida kumsaidia kwa Rais Samia Hassan Suluhu kupitia vyombo vyake vya Dola kukamata wahusika walioiba Sh milioni 200 za boda boda hao zaidi ya miaka minne iliyopita huku akiahidi donge nono la sh, milioni 1 kwa yoyote atakayesaidia watu hao.