Mil 640/- kuwezesha vikundi Mikindani

MANISPAA ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imetoa zaidi ya Sh milioni 640 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiliamali kwenye manispaa hiyo.
Akizungumza mkoani Mtwara wakati wa ghafla fupi ya kukabidhi fedha hizo kwa wajasiliamali hao, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya amesema utoaji wa fedha hizo ni maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Fedha hizo zilizotolewa kwa wajasiliamali hao ni ile mkopo wa asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Aidha jumla ya vikundi 58 vya wajasiliamali hao vimepatiwa mkopo huo ikiwemo vikundi 33 vya wanawake, vijana vikundi 22 pamoja na watu wenye ulemavu vikundi 3.
‘’Naomba niwaagize wakurugenzi wa halmashauri zingine ambazo bado hazijatoa mikopo kwenye wilaya hii kuhakikisha na wao wanatoa mikopo haraka iwezekanavyo kwenye halmashauri zao’’amesema Mwaipaya
Aidha wilaya hiyo ya mtwara ina halmashauri tatu ikiwemo Mtwara vijijini, halmashauri ya mji Nanyamba pamoja na manispaa hiyo lakini mpaka sasa manispaa ndiyo imekuwa ya kwanza kutoa mkopo huo.

Akitoa taarifa ya manispaa hiyo kuhusu kukabidhi mkopo kwa vikundi hivyo, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo Judidh Palangyo amesema ni imani yao kuwa vikundi hivyo vitaonyesha uwaminifu na mfano wa kuigwa katika urejeshaji mzuri wa mkopo ili kuwezesha waombaji wengine wenye uhitaji kuendelea kunufaika na mkopo hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga amewasisitiza wajasiliamali hao kuwa, wanapopatiwa mkopo huo wazingatie kurejesha wa wakati ili kuwezesha wananchi wangine wenye uhitaji kupata fursa ya kuchukua mkopo huo.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanavikundi wenzake, Mwenyekiti wa kikundi kinachojishughulisha na masuala ya ujenzi katika manispaa hiyo, Rasuli Abdallah ‘’Tunaishukuru sana serikali kwa kutupatia mkopo huu kwani tulikuwa na kiu cha mda mrefu kuhusu jambo hili’



