Mil 980/-kujenga maabara ya uchunguzi madini Geita

KAMPUNI ya Start Quality Consultancy Ltd inayoendesha maabara za madini za Start Mineral Laboratory (SML) imepanga kutumia kiasi cha Sh milioni 980 kujenga ujenzi maabara ya kisasa ya uchunguzi wa madini mkoani Geita.

Mkurugenzi Mtendaji wa SML, Simon Shinshi ametoa taarifa ya mradi huo Septemba 02, 2025 mbele ya viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 alipofika kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo.

Shinshi amesema ujenzi wa mradi huo unatekelezwa na mkandarasi kampuni ya PHB Design na Construction Ltd na utekelezaji ulianza Desemba 05, 2024 na unatarajiwa kukamilika Septamba 30, 2025.

Amesema utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 90 na umegharimu fedha kiasi cha sh milioni 780 za uwekezaji ambapo chanzo cha fedha za mradi ni michango ya wanahisa wa kampuni na mikopo kutoka taasisi za fedha.

“Mradi huu utakapokamilika utasaidia kutoa huduma bora ya uchunguzi wa sampuli za madini kwa teknolojia ya kisasa kwa wachimbaji wadogo, ili kuwawezesha kupata tija zaidi katika biashara ya madini”, amesema Shinshi.

Mradi huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya madini kwa kuwasaidia wachimbaji wadogo kuacha kusafiri umbali mrefu kifuata huduma ya maabara ya madini nje ya mkoa wa Geita.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2025, Ismail Alli Ussi amesema serikali ya awamu ya sita inatambua nafasi ya wawekezaji wazawa hivo itaendelea kuwaunha mkono kwa maslahi mapana ya umma.

Ifahamike kuwa Agosti 21, 2025 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alisema kuwa tayari serikali imeanza ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti na uchambuzi wa madini mkoani Geita itakayogharimu kiasi cha sh bilioni 3.5.

Mradi huo ni hatua kubwa inayolenga kuwainua wachimbaji wa madini Kanda ya Ziwa na kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa taifa.

Amesema maabara hiyo ni sehemu ya mpango wa serikali kujenga maabara tatu za kisasa za madini nchini ambapo maabara nyingine itajengwa Chunya mkoani Mbeya na maabara kubwa zaidi kimataifa itajengwa jijini Dodoma.

Mavunde amesema chini ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) maabara ya GST kanda ya ziwa itahudumia mikoa ya kimadini ya Geita, Mbogwe, Kagera, Mwanza, Kahama, Mara na Shinyanga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button