Mipangomiji wafundwa kutekeleza majukumu kwa weledi

ARUSHA; Katika kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa masuala ya mipangomiji nchini, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia idara ya Maendeleo ya Makazi, inaendesha kikao kazi kwa maofisa mipangomiji wa mikoa ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika mkoani Arusha kuanzia Sept mosi, .2025 na kinatumika kukumbushana maadili kwa maofisa hao, muongozo wa upangaji na utekelezaji mipango ya uendelezaji miji, umuhimu wa kufanya ukaguzi wa matumizi ya ardhi pamoja na uidhinishwaji kazi za mipangomiji kwenye mfumo wa e-ardhi.
Idara ya Maendeleo ya Makazi moja ya majukumu yake ni kupanga miji vizuri pamoja na kusimamia uendelezaji wake (Development control).
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratias Kalimenze amewaambia washiriki wakati wa kufungua kikao hicho kuwa wao ndiyo waliobeba dhamana nzito ya kuhakikisha ulimwengu unakuwa na sehemu salama ya kuishi.
‘’Tumepewa dhamana ya kuhakikisha tunawafanya watu waishi katika mazingira ambayo ni mazuri, ni mipango yetu ndiyo inayoongoza namna gani watu wataishi, watafanya kazi, ajira zitakavyopatikana, tutalindaje rasilimali zitumike kizazi na kizazi, nishati itumikeje,’’ amesema Kalimenze na kuongeza:
‘’Jukumu mlilokuwa nalo ni kubwa na katika kulitekeleza hilo ni lazima muwe na weledi wa hali ya juu, nidhamu katika kutekeleza majukumu pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kuongoza utekelezaji majukumu ya kila siku ili msisababishe ajali kwa wale mliopewa majukumu ya kuwafanya waishi katika dunia kwa furaha,” amesema..
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6